Prof. Sospeter Muhongo |
WAZIRI wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ametoa
somo kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza pamoja na kuwa na rasilimali nyingi ikiwemo
maji, madini na ardhi yenye rutuba lakini Jiji la Mwanza bado limetajwa
kuendelea kuwa tegemezi na watu wake kuendelea kuwa masikini.
Akizungumza
na wadau wa sekta ya Madini na Umeme katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la
Mwanza leo amesema amesikitishwa na kitendo cha watu kupoteza muda mwingi kwenye
mambo yasiyo na maana ikiwemo kukesha kwenye malumbano ya kisiasa badala ya
kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa manufaa ya kujiongezea kipato na
kusaidia kukuza uchumi wa Taifa.
Msikilize kwa Kubofya play...
Msikilize kwa Kubofya play...
Kusanyiko la wadau wa sekta ya Madini na Umeme katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza leo. |
Waziri
huyo amewataka wananchi pia kuhakikisha wanaimarisha ulinzi kwenye miundombinu
ya shirika la umeme (TANESCO) isihujumiwe na watu ambao hawapendi maendeleo na
wasiotambua umuhimu wa nishati ya umeme kwa kuachia wizi wa mafuta ya Transfoma
na nyaya za umeme kwenye maeneo yao kisha kuanza kulalamikia TANESCO jambo
ambalo linaonyesha jinsi watu walivyo kosa uzalendo.
Ameeleza kuwa serikali pia imeanzisha utaratibu wa kugharamia miundombinu ya kuwafikishia
umeme wateja wake kwa miradi inayopata ruzuku kutoka Mfuko wa Nishati Vijijini
(REF) na mpango huo utapunguza gharama za kuunganisha umeme kwa wastani wa
asilimia 80 kulingana na idadi ya nguzo na mfumo utakaotumika huku idadi ya awali
ya wateja watakaofaidika watakao unganishiwa na umeme kupitia mpango huo kuwa
100,000 nchi nzima.
“Kupitia
mradi huu Halmashauri zihakikishe zinashirikiana na wananchi kuunganisha umeme
kwenye shule za sekondari za kata kutokana na unafuu wa gharama hizi ambapo
shule yenye madarasa nane gharama yake
ni shilingi milioni 4, Bweni milioni 14 na vituo vya afya milioni 12 hivyo
amewashauri madiwani kutenga fedha kuweka umeme kwenye shule hizo badala ya
kusubili serikali kuwafanyia” alisema.
Ramani ya Mradi wa uzalishaji umeme wa gesi asili kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songo Songo hadi Dar es salaam wa bomba la urefu wa kilomita 532 utakaogharimu kiasi cha dola 1,2253 ukikamilika ndani ya miezi 18 chini ya ufadhili wa nchi ya China.
Ramani na maainisho ya sehemu mbalimbali za vijiji hapa nchini ikionyesha miundombinu ya kuwafikishia umeme wateja wake kwa miradi inayopata ruzuku kutoka Mfuko wa Nishati Vijijini (REF)
Mchangiaji..
Mswali na uchangiaji nao ulikuwemo.
Kuhusu wachimbaji wadogo wa madini Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa serikali imeamua kuwa ni lazima wachimbaji hao kuchimba kisasa na haiwezekani kuendelea na uchimbaji wa nyenzo duni na itahakikisha wachimbaji hao wanalipa kodi huku serikali imetenga kiasi cha bilioni 8.9 kwa ajili ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata vifaa vya kisasa,kuwatafutia masoko ya uhakika na kuwapatia leseni za uchimbaji.
Msikilize kwa Kubofya play...
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.