ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 22, 2012

TANZANIA YASIFIWA KWA KUONGEZA UFANISI KATIKA BANDARI ZAKE

Mwakilishi wa Tanzania Phares Magesa akiwasilisha mada inayohusu mfumo mpya wa eSWS katika mkutano huo.

Ndugu Magesana washiriki wengine wakifuatilia majadiliano


Ndugu magesa akibadilishana mawazo na mshiriki wa mkutano huo kutoka Wizara ya viwanda na Biashara ndugu Manumbu.
Katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia Uchumi Afrika (UNECA) uliokuwa unafanyika Moroni, Comoro 20-21 Novemba, 2012, Mkutano wenye lengo la kuendeleza biashara bila kutumia karatasi "Advancing Paperless Trade in Eastern Africa".

Tanzania ilisifiwa na wasemaji wengi wa mkutano huo kutokana na juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na kuongeza ufanisi katika bandari zake.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa serikali na wataalamu wa masuala ya usafirishaji na Teknolojia ya habari na mawasiliano(Tehama) kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na visiwa vyote vya bahari ya hindi.

Mmoja wa wachangiaji mada katika mkutano huo ndugu Hamidou M'Homa ambaye ni Rais wa Chama Cha watumiaji wa huduma Comoro, alisema kwa kipindi cha karibuni ameona ufanisi umeongezeka katika bandari za Tanzania na akatoa pongezi nyingi kwa jitihada zinazofanywa na serikali na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha huduma.

Msemaji wa Tanzania katika mkutano huo Ndugu Phares Magesa alipokea salamu hizo za pongezi na kuelezea jitihada mbali mbali zinazofanywa na TPA na Serikali katika kuboresha huduma katika badari zetu. Moja ya jitihada hizo kwa upande wa Teknolojia ni kuanza matumizi ya mifumo ya kisasa ya kuhudumia mizigo na meli ambapo sasa watumiaji wa huduma za meli na mizigo wanaweza wakafanya kazi kutokea maofisini kwao badala wote kwena bandarini hivyo kupunguza msongamano bandarini na kurahisisha utuoaji huduma.

Jitihada nyingine ni Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wote wa bandari kuamua kuharakisha ununuzi na ufungaji wa mfumo wa kisasa wa kutoa huduma zote za kibiashara ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini , mfumo huu unaitwa Tanzania Electronic Single Window System(eSWS), ndugu Magesa aliulezea kwa kirefu mfumo huu na jinsi utakavyorahisisha huduma za kibandari na kiforodha. Mfumo huu unatarajiwa kupunguza muda wa kukaa mizigo bandarini na kufikia siku 5 au chini ya hapo. 
Kwa sasa bandari zote chini ya jangwa la sahara ukiacha Durban ya Afrika Kusini, zinatumia zaidi ya siku 10 na zingine hadi 20. Hivyo basi kwa kuweka mfumo huu pamoja na jitihada nyingine za kuboresha miundombinu ya usafirishaji na utoaji huduma, Tanzania itafikia malengo yake katika miaka michache ijayo ya kufanya bandari ya Dar es Salaam kuwa moja ya bandari bora duniani na hii itachochea kukua kwa uchumi wa Tanzania na kuongeza mapato ya Serikali.

Nachukua nafasi hii kuwaomba wadau wote sasa watoe ushirikiano mzuri ili mifumo hii iweze kuleta tija na kutoa mrejesho chanya ili kuboresha huduma kwa faida ya nchi yetu na wananchi wote kwa jumla .

Phares Magesa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.