Mashindano ya Robert cup ya mpira wa kikapu kwa mwaka huu 2012 yamefanyika kwa kuwakutanisha wachezaji walionza kucheza kikapu kuanzia mwaka 2001 kurudi nyuma dhidi ya walianza kucheza kuanzia mwaka 2002 mpaka sasa.
Mashindano hayo kwa miaka ya nyuma yalikuwa yakifanyika kwa mtindo wa ligi ama bonanza lakini kwa mwaka huu wachezaji waliomba kucheza katika mtindo tofauti wa wakongwe na chipukizi.
Katika mechi hii, timu ya chipukizi (wa leoleo) iliifunga timu ya wakongwe vikapu 48 kwa 33. Katika robo ya kwanza (12 kwa 10), ya pili (13 kwa 06), ya tatu (10 kwa 09) na robo ya 4( 13 kwa 08), katika mechi hii kwa upande wa washindi, Sebastian marwa aliongoza kwa kuifungia timu yake vikapu 12 akifuatiwa na Baraka lucas na Henrico maengela waliofunga vikapu 8 kila mmoja, kwa upande wa wakonge selemani abdula aliongoza kwa kufunga vikapu 17 akifutiwa na amri Mohamed, Shomari Almas na Benson Nyasebwa walifunga vikapu 5 kila mmoja.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa kikapu wa chuo kikuu ya mt. Augustino (SAUT), ulichezwa sambamba kuwaaga wachezaji waliokuwa wanachuo wahitimu wa SAUT ambao walishiriki mashindano ya Robert cup kwa miaka ya 3 nyuma wakiwa wachezaji wa timu ya chuo. Wachezaji hao ni Baraka Lucas na Benson Nyasebwa ambaye huyu ameshiriki mashindano haya kwa zaidi ya miaka kumi akitokea timu ya mwembeni musoma na wakati akiwa mwanachuo wa chuo cha ualimu butimba. Kwa mwaka huu mashindano haya yanafikisha miaka 11.
Akiongea kwa njia ya simu, mama mzazi wa Robert ambaye pia ndie mlezi wa chama cha mpira wa kikapu mwanza (MRBA), mh. Gaudentia M. kabaka (waziri wa kazi na maendeleo ya vijana) aliwataka vijana kutumia michezo hasa mpira wa kikapu katika kupambana na magonjwa mabalimbali kama vile maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi ama kupambana na malaria kama ilivyokuwa kauli mbiu ya mpira wa kikapu kwa mwaka huu (basketball vs HIV/AIDS and Malaria) na pia alisisitiza michezo ni sehemu ya kufahamiana na kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa washiriki wenzako.
Wachezaji walioshiriki walitoka katika timu za mpira wa kikapu za Bugando planet, bugando heat, bugando worrious, butimba spiders, mwembeni (musoma), dolphin pasiansi, SAUT, Mwanza eagles, st. francis na nyakato Brandon.
Ligi ya Robert cup huchezwa kwa lengo la kumkumbuka marehemu Robert Chacha Kabaka aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 2000 jijini dar, alikuwa ni mmoja ya waanzilishi wa timu ya mpira wa kikapu ya butimba spiders.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.