ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 3, 2012

TAFAKARI LA BULABO NA UTALII WA MWANZA



Hello,

Kwanza kabisa ningependa kuanza kwa kujitambulisha, naitwa Shinyela, Isaac ni mwanafunzu wa Architecture mwaka wa 4 chuo cha Ardhi Dar es salaam. Pia ningependa kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya katika blogu yako. Mimi ni moja ya wapenzi wa blogu hilo ambalo ni moja ya blogu chache ambazo zinatupa taarifa za matukio mbali mbali yanayojiri mjini kwetu Mwanza.

Katika soma soma zangu sikumoja, nilitembelea blogu yako nikakuta habari moja ambayo ilinifurahisha sana lakini pia ilinipa changamoto za kimawazo kwani kila jambo katika ulimwengu huu ni fursa kwa watu makini wenye nia na mawazo bora. Naamini katika watu, hususani vijana ambao wanania na mitazamo huru. Naamini kuwa wewe ni miongoni mwa watu muhimu ambao kama tutashirikiana katika hili pamoja na wadau wengine, tunaweza fanya jambo ambalo tutajivunia na pia tutanufaika hapana shaka.

Sifahamu wewe ulichukuliaje habari ya Bulabo ambayo uliibandika katika blogu yako siku kadhaa zilizopita, binafsi nilifurahi sana kwani niliona watu na utamaduni. Mimi ni msukuma, nilifurahi sana kuona watu wa jamii yangu wakiserebuka kusherehekea msimu wa mavuno kwa ngoma za kitamaduni. Lakini pia niliona fursa ambazo, mimi, wewe pamoja na wadau wachache wengine ambao nime/nita wahusisha katika hili tunaweza kuzitumia.

Bulabo ni festival kama ilivyo Sauti za busara zanzibar na ZIFF. Lakini kama mjasiriamali unapaswa ujiulize, kwa nini ZIFF na Sauti za Busara ni matukio maarufu na makubwa yanayo fahamika ulimwenguni kote kwa sasa na Bulabo si kitu bali Ngoma tu? wakati katika uhalisia Bulabo ilipaswa kuwa tamasha kubwa kuliko yote haya kwani ilikuwepo kabla ya ZIFF na Sauti za busara. Nilichogundua ni kwamba, Bulabo imekosa wabunifu wazalendo.

Kwa kufahamu hilo, niliona pana haja ya kuatafuta watu wenye mtazamo kama wangu, wabunifu kama wewe na walio na uzalendo wakutosha. Naamini sijakosea kukuandikia barua pepe hii kuomba ushirikiano wako katika event hii, naimani pamoja tunaweza shirikiana, tukaunda 'EVENT ORGANIZATION TEAM' ambayo ita 'MODERNIZE' Bulabo kwa kuitangaza, kuongeza 'VARIETY' ya shughuli na kuisanifu ili iendane na soko la utalii wa nje na ndani kwa sasa na pia kutafuta wahisani na makampuni yatayo changia kuwezesha shughuli hii. Naomba uitazame Bulabo kama fursa ya kiuchumi kwetu na kwa mkoa kiujumla, pia ni nafasi ya kuutangaza mkoa wetu wa Mwanza kimataifa.

Ni muda sasa tumekuwa tukisema 'TUKUZE UTALII WA MWANZA' lakini bado utalii wa mkoa wetu umedumaa. Naamini namna pekee ya kukuza utalii wa mkoa wetu ambao kwa uhalisia una uhaba wa mbuga za wanyama ni kubuni vivutio mbadala vya utalii. Ni lazima tuachane na dhana ya utalii wa mali asili kama aina pekee ya utalii uliopo, Tazama Italy na Zanzibar, watu hawaendi kutazama wanyama, wanakwenda kuona Architecture na maendeleo ya makazi. Hii ndio sababu tunatunza miji kama mji mkongwe, Florence na Venice. Lakini pia kuna utalii wa tamaduni, mamilioni ya watu kila mwaka huenda India kushangaa wahindi wakioga katika mto Ganges. Vivyo hivyo, kwanini nasisi tusiwape watu sababu ya kuja kuona utamaduni wa Kitanzania? Namaanisha tuifanye Bulabo iwe zaidi ya tukio la Wasukuma, Bulabo inaweza kuwa tukio la kitaifa na kimataifa lenye mizizi yake kwenye utamaduni wa Msukuma.

Kuna mengi ya kuzungumza, lakini naomba utafakari haya machache, kisha kama unaona umevutiwa tafadhali tuwasiliane.

Shinyela, Isaac

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Hilo neno kaka nimekuwa nikijiuliza siku nyingi sana finally here we go now..

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.