ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 10, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KAMANDA AELEZA WALIVYOJIFICHA MAKABURINI BAADA YA KUFANYA MAUAJI

Abdurahman Ismail aka Dulla (28) ambaye ni mkazi wa Mkudi Ghana jijini Mwanza ambaye ni mdogo wa watuhumiwa  Muganyizi Michael Peter aliyedaiwa kumfyatulia risasi marehemu Barlow alieleza jinsi walivyo tekeleza unyama wao na kwenda kuficha radio call na funguo za gari kwa kutupa katika tankila maji taka katika eneo la Nyashana kwenye nyumba ambayo haina mahusiano yoyote na hao watuhumiwa bali kwa lengo la kuhakikisha vitu hivyo havipatikani kabisa.

Watuhumiwa wawili waliofungwa pingu wakiwa wameshikiliwa na makachero wa jeshi la polisi waliovalia kiraia wakiwaonyesha kwenye shimo la maji taka eneo ambalo walitupa Radio call pamoja na funguo za gari la aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza marehemu Liberatus Barlowpo. 

Hawa ni watuhumiwa wawili kati ya saba wanaoshikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kutoka kushoto ni Abdurahman Ismail aka Dulla (28) ambaye ni mkazi wa Mkudi Ghana jijini Mwanza na Amos Abdalah (32) mkazi wa mji mwema Wilayani Ilemela ambaye pia aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha mwaka 2006 katika gereza la Butimba, kabla ya kukata rufaa na kushinda mwaka 2010 ambapo aliachiliwa huru. 
Watu hao walitumbukiza radio call hiyo na funguo za gari kupitia bomba linaloonekana kulia la kupitishia hewa ya maji taka na hapa ni harakati za kutindua mlango wa shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la  mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza (RCO) Joseph Konyo akijiandaa kuchungulia ndani ya shimo la maji taka lililotajwa kuwa na radio call na ufunguo wa gari la vilivyokuwa vikitumiwa na marehemu Barlow siku ya tukio la  mauaji yake eneo la minazi mitatu Kitangili wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Shimo lenyewe.


Picha ya ndani ya shimo hilo..

Radio call kabla haijafanyiwa usafi...

Funguo za gari  zikifanyiwa usafi..

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza (RCO) Joseph Konyo akionyesha betri ya radio call iliyotenganishwa na radio call yenyewe wakati akizungumza na vyombo vya habari ikiwemo blog ya G. Sengo

Hivi ni baadhi ya vitu vilivyokamatwa nyumbani kwa watuhumiwa hao vikiwemo vyeti vya kughushi, pasipoti  na picha za utambulisho wa kughushi wa kipolisi, simu zaidi ya nne zenye laini zake na laini nyingine za ziada kwa mitandao tofauti, sare za moja kati ya makampuni ya ulinzi Mwanza, kofia zenye nembo ya jeshi la Polisi na kadhalika...

Panga na nondo ni moja kati ya vielelezo...

Sare za moja kati ya makampuni ya ulinzi....

Tv, sub woofer ambavyo vinatajwa kuwa ni mali ya wizi vikiwa sambamba na buti na viatu hivi ni sehemu tu ya vielelezo vilivyonaswa kwa watuhumiwa hao.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. I do not know whether it's just me or if perhaps everybody else experiencing issues with your blog. It seems like some of the text in your posts are running off the screen. Can somebody else please comment and let me know if this is happening to them too? This could be a problem with my browser because I've had this happen
    before. Cheers

    http://api.mybuzzboard.com/forums/topic/confessions-with-regards-to-a-twitter-pinger/
    http://apollo.friendsacademy1810.org/groups/latin/wiki/5d44e/Mishap_Twitter_Concerning_Twitter_Automaticaly.
    html
    http://amateur-swingers-posts.com/forums/profile.
    php?mode=viewprofile&u=1634293
    http://apple-obzor.ru/node/18711
    http://anicomu.com/userinfo.php?uid=10099

    Feel free to visit my homepage: basketball trick shots

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.