Viongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wametakiwa kuenzi juhudi mbalimbali zilizo fanywa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan aliyefariki dunia ghafla jana za kutatua migogoro iliyokuwa ikijitokeza duniani.
Rai hiyo imetolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, Profesa Anna Tibaijuka aliyetumikia shirika hilo kwa kipindi cha miaka 10 aliapozungumzia kifo cha Annan.
Profesa Tibaijuka ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini ametoa kauli hiyo wakati akielezea anavyomfahamu marehemu Annan amesema alikuwa mchapa kazi na alikuwa hayumbishwi katika kutoa uamuzi ya migogoro iliyokuwa ikijitokeza duniani.
Profesa Tibaijuka amesema hayati Annan alifanya kazi bila kutanguliza ubaguzi wa rangi, jinsia na ukabila na ndiye aliwateua Waafrika na watu wengine kutoka katika nchi masikini kushika nafasi za juu za uongozi ndani ya Umoja wa Mataifa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.