ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 20, 2018

RC MAKONDA KUJENGA VIWANJA VITANO VYA RC MAKONDA KUJENGA VIWANJA VITANO VYA BASKETBALL

 NA ZEPHANIA MANDIA/G.SENGO TV.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amefanikiwa kupata wadau watakaojenga Viwanja 5 vya Basketball (in door) kwenye wilaya zote Tano za Mkoa huo kwa lengo la kuimarisha sekta ya michezo. 

RC Makonda amesema Viwanja hivyo pia vitaweza kutumika kwa Michezo zaidi ya Mitano ikiwemo Ngumi, Mieleka, Volleyball na Table Tennis ambapo kila kiwanja kitakuwa na uwezo wa kupokea Mashabiki 3,000.

Aidha RC Makonda amemchagua Mchezaji maarufu wa Basketball Bwana Hasheem Thabit kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo ujenzi wa kiwanja kimoja peke inakadiriwa kugharimu Kati ya Shilling Million 300 hadi 500.

Uamuzi wa RC Makonda kuja na mkakati wa kujenga Viwanja hivyo ni baada ya kubaini uwepo wa idadi kubwa ya vijana wanaopenda michezo kwenye mkoa wake lakini wanashindwa kufanyia kazi vipaji vyao kutokana na changamoto za ubovu wa miundombinu ya viwanja vya michezo. BASKETBALL*.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amefanikiwa kupata wadau watakaojenga Viwanja 5 vya Basketball (in door) kwenye wilaya zote Tano za Mkoa huo kwa lengo la kuimarisha sekta ya michezo. 

RC Makonda amesema Viwanja hivyo pia vitaweza kutumika kwa Michezo zaidi ya Mitano ikiwemo Ngumi, Mieleka, Volleyball na Table Tennis ambapo kila kiwanja kitakuwa na uwezo wa kupokea Mashabiki 3,000.

Aidha RC Makonda amemchagua Mchezaji maarufu wa Basketball Bwana Hasheem Thabit kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo ujenzi wa kiwanja kimoja peke inakadiriwa kugharimu Kati ya Shilling Million 300 hadi 500.

Uamuzi wa RC Makonda kuja na mkakati wa kujenga Viwanja hivyo ni baada ya kubaini uwepo wa idadi kubwa ya vijana wanaopenda michezo kwenye mkoa wake lakini wanashindwa kufanyia kazi vipaji vyao kutokana na changamoto za ubovu wa miundombinu ya viwanja vya michezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.