ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 25, 2018

MISRI LAKUVUNDA HALINA UBANI.


GSENGOtV

Msala umezidi kuisaka Afrika kwa timu zake kuendelea kupoteza dakika za mwisho mara baada ya Misri kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Saudi Arabia leo.

Misiri ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lake mnamo kipindi cha kwanza katika dakika ya 22 kupitia kwa nyota wake, Mohamed Salah na baadaye wapinzani wakasawazisha kwenye dakika ya 45+6 kwa njia ya penati kupitia kwa Salman Al-Faraj.

Matokeo hayo yalienda mpaka mapumziko yakiwa ni 1-1.

Na kipindi cha pili kilianza kwa Misri kuonekana imeelemewa na Saudi ambapo kuelekea dakika za mwisho mwa mchezo, mchezaji Salem aliweza kutikisa nyavu za Misiri zikiwa zimesalia dakika 5 kumalizika.

Matokeo hayo yanakuwa hayana manufaa kwa timu zote mbili ambazo zilikuwa kundi A na kuanzia kesho zitakuwa zinajiandaa kuanza kurejea makwao.

Katika msimamo wa kundi A, Misri imeshika mkia ikiwa na alama 0 huku Saudi Arabia wakiwa na 3 kutokana na ushindi wa leo.

Wakati huo Uruguay walioibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Urusi leo wamekalia nafasi ya kwanza wakiwa na alama 9 huku Urusi wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 6.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.