"Mwaka 2014 Tanzania ilipitisha rasmi Sera ya Elimu na Mafunzo. Sera hiyo ni maboresho na mwendelezo wa Sera ya awali ya mwaka 1995. Lengo kuu la Sera hii mpya ni kuwa na watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka zaidi katika maendeleo ya taifa na kuhimili ushindani kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko. Sera ya elimu ya mwaka 2014 inatambua na kuhimiza umuhimu na ushirikishwaji wa sekta binafsina taasisi za kijamii katika kuchangia elimu nchini hasa ikizingatiwa kuwa kanisa limekuwa kwa muda mrefu ni mdau katika harakati za kutoa elimu na huduma nyingine za jamii." Alisema Mgeni Rasmi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Jude Thadeus Ruwaich wakati akizungumza kwenye Mahafali ya Chuo cha Mtakatifu Augustine yaliyofanyika katika viwanja vya Raila Odinga Malimbe jijini Mwanza..
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.