ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 12, 2017

WANAFUNZI 26 WASHINDWA KUFIKIA NDOTO ZA KUENDELEA NA MASOMO KUTOKANA NA KUPATA MIMBA.

Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya  Mtoto wa kike Duniani ambayo Katika Wilaya ya Geita yamefanyika kwenye Kata ya Kasamwa.
Maandamano ya wanafunzi kuelekea kwenye viwanja kwaajili ya sherehee za siku ya Mtoto wa Kike.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakiwa kwenye sherehee ya siku ya mtoto wa kike.
Afisa maendeleo ya Jamii Majagi Maiga Akisoma taarifa ya maendeleo ya mtoto wa kike katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike Duniani.
Meza kuu ikiongizwa na Mkuu wa Wilaya ikisikiliza taarifa ya Afisa maendeleo ya jamii.
Baadhi ya wanafunzi wakilisakata lumba wakati wa sherehee hizo.
Mbunge wa Geita Mjini,Costantine Kanyasu na Diwani wa Kata ya Kanyara Enock Mapande wakilisakata Lumba.
Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Costantine Kanyasu akizungumza na wanafunzi pamoja na wananchi ambao walijitokeza katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita (Kushoto)Mwl Herman Kapufi na Mgeni Rasmi(Kulia)Jesca Emmanuel wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini.
Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali la Plan International Mkoani Geita,Mekiseri Madubi akizungumza namna ambavyo shirika limeendelea kupinga ukatili dhidi ya watoto wa kike.
Akiendelea kuchukua matukioa kwa  kutumia simu Janja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinal akielezea tatizo lilivyo la mimba kwa wanafunzi ndani ya halmashauri hiyo.

Mgeni Rasmi ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Kasamwa ,Jesca Emmanuel ,akielezea changamoto ambazo zimeendelea kumkabili mtoto wa kike.PICHA NA JOEL MADUKA.


Ikiwa leo Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani hali bado sio shwari  kutokana na tatizo la mimba za utotoni kwa watoto wa kike ni moja ya changamoto ambazo zinaathiri maendeleo yao.

Tatizo hilo bado ni kubwa na linahitaji juhudi ya pamoja kukabiliana nalo,kitaifa tatizo la mimba za utotoni lipo kwa asilimia 27,Mkoa wa Katavi umeathirika kwa asilimia 36.8,Tabora asilimia 27,Simiyu 32.1%,Geita 31.6%na Shinyanga 31.6%

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ambayo yamefanyikia kwenye Kata ya Kasamwa ,Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya Mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinaly  amesema Wanafunzi 26 wakiwemo wa shule za sekondari na msingi   wameshindwa kufikia ndoto zao za kuendelea na masomo kutokana na kupatiwa ujauzito katika kipindi cha January hadi Oktoba mwaka huu katika halmashauri ya Mji wa Geita.

Ameendelea kusema kuwa halmashauri hiyo ina shule za sekondari   10 na kwa mwaka huu jumla ya wanafunzi 18 wamepatiwa mimba kutoka kwenye shule hizo na kwa upande wa shule za msingi 47 na wanafunzi 8 wamekatisha masomo kwa sababu ya kupata mimba.

Ameongeza kuwa Kata ya kasawa haipo salama kutokana na shule ya sekondari  iliyopo kwenye kata hiyo  wanafunzi wanane kupata mimba kati ya kumi (10) kwenye Halmashauri hiyo.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Kasamwa ,Jesca Emmanuel ,amesema kuwa kumekuwepo na desturi ya kutokuripotiwa kwa wasichana ambao wanabebeshwa mimba na kuwa wasili hali ambayo inaathiri takwimu za wanafunzi ambao wamepata ujauzito.

Mbunge  wa Jimbo la Geita,Mjini Costatine Kanyasu ameendelea kuwasisitiza wazazi kuweka malezi bora kwa watoto  wa kike pamoja na kuwatengenezea mazingira ambayo yatamsaidia mtoto kuwa na msimamo ambao utamsaidia kutimiza ndoto zake.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema”Tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.