ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 29, 2017

RAIS MAGUFULI KUZINDUA MIRADI MINNE MWANZA OCTOBER 30

NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGOBLOG


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, October 30 mwaka huu anatarajiwa kuwasili Jijini Mwanza kwa ajili ya ziara ya siku mbili, ambapo pamoja na mambo mengine atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.


Akitoa taarifa ya ujio wa Rais Dk. Magufuli, mkuu wa mkoa wa Mwanza Mwanza John Mongela, amesema baada ya Rais kuwasili atazindua daraja la kisasa la kisasa la watembea kwa miguu la Furahisha na kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Nyakato.


Amesema mbali na shughuli hizo vilevile atazindua kiwanda cha Dawa cha Prince Pharmaceutica kilichopo Buhongwa pamoja na kufungua kiwanda cha Victoria Moulders and Polybags kilichopo Igogo.


Kutokana na ujio huo Mongela amewaomba wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Rais Dk. Magufuli, atakapokuwa akizindua miradhi hiyo na kisha kuzungumza na Wananchi.


Ziara ya Rais Dk. John Pombe Magufuli, inatarajiwa kukamilika October 31 mwaka huu, baada ya kukamilisha shughuli zote za uzinduzi wa miradi ya maendeleo Jijini Mwanza, zinazolenga kuboresha maisha ya watanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.