ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 18, 2017

PICHA ZA LISSU SASA NJE NJE

Kwa mara ya kwanza picha za mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu zimeanza kuonekana hadharani baada ya kuwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)tangu september 7.

Katika picha hizo ya kwanza juu ameonekana akiwa mwenye tabasamu kama ada yake akionesha ishara ya vidole viwili nje wakati akipata upepo.
Na picha ya pili ameonekana akiwa ameketi katika kiti cha mapumziko pembezoni mwa kitanda chake cha hospitali ya Nairobi nchini Kenya, mguu mmoja akiwa ameuning'iniza kwenye kiti kingine huku akipunga mkono huku akitabasamu akiashiria kuwasalimu ndugu jamaa na marafiki poote ulimwenguni.

Jana jumanne kwenye mkutano na wandishi wa Habari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alimtaja mbunge huyo kuwa anaendelea vizuri huku akisema kuwa muda wowote kuanzia hiyo jana picha za Lissu zitaanza kuonekana kwani walifanya hivyo kwasababu za kiusalama.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.