Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka
akizungumza na wananchi katika moja ya mikutano yake.
Katibu wa Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Method
Mselewa akizungumza na baadhi ya walemavu hawapo pichani katika kituo hicho kabla ya
kukabidhi rasmi vyelehani vine ambayo vitaweza kuwasaidia katika kujikwamua
kiuchumi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu
(SHIVYAWATA) Wilaya ya Kibaha mjini Mohamed Mlanga ambaye ni mlemavu wa macho
akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kupokea
vyelehani hivyo.
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Kibaha Regina
Mgovellah akizungumzia lengo la halmashauri ya Kibaha mji katika kuwasaidia
walemavu wa aina mbali mbali.
Baadhi ya walemavu pamoja na viongozi mbali mbali
wa serikali na viongozi wa CCM kutoka jumuiya mbali mbali wakiwa katika picha
ya pamoja nje ya jengo hilo la kituo cha walemavu mara baada ya kumalizika kwa
halfa fupi za ugawaji wa vyelehani.
(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU,
KIBAHA (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
KITUO cha watu wenye ulemavu wa aina mbali mbali kilichopo
kwa Mfipa katika halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani kimepatiwa msaada wa vyelehani vinne kwa lengo
la kuweza kuwasaidia katika kuendeshea shuguli zao za ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi, kupambana na wimbi la
umasikini sambamba na kukabiliana na changamoto zinazowakabili hususan
upatikaji wa mitaji na vitendea kazi.
Msaada huo ambao umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha
mjini Silvestry Koka ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa ya
kuhakikisha anaweka mipango madhubuti ambayo itaweza kuwawezesha walemavu
waweze kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe kupitia shughuli za ujasiriamali na kuweza kupata
kipato ambacho kitawasaidia kujikimu kimaisha.
Akikabidhi kwa niaba
msaada huo katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kituo hicho
Katibu wa Mbunge huyo Method Mselewa
amesema kuwa msaada huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwani utaweza
kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika
shughuli mbali mbali za ushonaji ambazo zitawapa fursa ya kujiingizia kipato na
kujikwamua kiuchumi.
Katibu huyo alisema kuwa ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha
mjini inatambua uwepo wa kundi la watu wenye ulemavu hivyo wataendelea
kushirikiana nao bega kwa bega katika kuwawezesha katika mambo mbali mbali
ikiwemo kuwapatia mitaji pamoja na vitendea kazi ambavyo vitaweza kuwa ni
mkombozi mkubwa katika suala zima la kuleba mabadilo ya kimaendeleo.
“Mimi nimekuja kwa niaba
ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa hivyo ameniagiza kama katibu wake
nije kutoa msaada huu wa vyelehani vine kwa kituo hiki cha walemavu wa aina mbali mbali hivyo ninachokiomba
viongozi wanaohusika kuhakikisha kuwa wanavitunza vifaa hivi ili viweze
kuwasaidia na wengine wenye mahitaji katika siku za mbeleni na kuleta tija
zaidi katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na vikundi husika,”alisema
Katibu huyo.
Naye Mwenyekiti wa shirikisho
la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA)
Wilaya ya Kibaha mjini Mohamed Mlanga
ambaye ni mlemavu wa macho amempongeza Mbunge Koka kwa msaada huo wa vyelehani
na kumwomba Rais wa awamu ya tano Dk.John Pombe Magufuli kuwasaidia kwa hali na
mali walemavu wote nchini kuwawezesha katika kuwapatia mitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za
ujasiriamali.
Kwa upande wake Afisa
maendeleo ya jamii kata ya Kibaha Regina Mgovellah amesema kuwa lengo kubwa la
ujenzi wa kituo hicho cha walemavu ni kwa ajili ya kuwakutanisha kwa pamoja na
kuwapatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha
sambama na kuwasaidia katika kuwapatia
mahitaji mengine ya msingi.
HALMASHAURI ya mji Kibaha imeamua kuwajengea walemavu kituo
hicho maalumu kwa ajili ya kuweza kuendeshea shughuli zao mbali mbali za ujasiriamali ambapo kwa sasa
wameshaanzisha miradi mbali mbali ya ushonaji,kilimo cha mboga mboga ili kuweza kujikwamua kimaisha na kuleta mabadiliko
chanya ya kimaendeleo ambapo kwa sasa kituo hicho kina jumla ya idadi ya
walemavu 687.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.