ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 1, 2017

NA ZEPHANIA MANDIA WA G.SENGO TV

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameongoza shughuli za kufanya usafi katika Soko kuu mkoani hapa.
Zoezi hilo limefanyika Jumamosi ya tarehe 29 kutimiza ada iliyo kama sehemu ya utaratibu wa zoezi hilo kufanyika kwa dhati kila jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Kutokana na baadhi ya wapiga debe kuibuka asubuhi hiyo kwenye shughuli huku wakiwa chakari na vilevi, baadhi yao wakiweweseka kuonekana kuwa wamezidiwa, hapo ndipo Mhe. Mabula akalazimika kutoa msisitizo kwa kuwataka makonda na wapiga debe kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na unywaji wa pombe zilizo katazwa aina ya viroba, vilevi ambavyo hupelekea wao kuwa duni na kikwazo kwa abiria.
Aidha Mbunge huyo wa Nyamagana amewaasa wadau hao wa usafiri na usafirishaji hususani makonda na wapiga debe kuvaa sare zao wakati wa kazi ili kutambulika na pia kuacha kutumia kauli chafu kwa abiria, suala ambalo limekuwa likizua mitafaruku na hata pengine madhara.
Ili kutimiza adhma ya zoezi hilo kuwa endelevu na lenye mafanikio Mabula amewaahidi wadau hao kuwasaidia vifaa vya kufanyia usafi. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.