ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 9, 2017

BASATA SASA WATINGA HADI HARUSINI MWANZA.

Akijibu kilio cha wasanii hao, Afisa Habari mkuu wa BASATA AGNESS KIMWAGA amewataka wasanii kuingia mikataba ya kisheria ili kuepuka kutapeliwa.

Bi. Agness amesema kuwa msanii akitengeneza kazi yake kabla ya kuipeleka sokoni ni lazima ipite BASATAisikilizwe, ishauriwe, kama haifai itarudishwa kufanyiwa marekebisho, kama itafaa itapewa barua kwenda TRA iruhusiwe rasmi kuingia sokoni. Pamoja na suala la vibali kwa makusanyiko mbalimbali ikiwemo harusi, hafla mbalimbali, mikutano na sherehe mbalimbali ndani ya viwanja na kumbi za sherehe nalo likaibuka. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Wasanii wa filamu,ngoma za asili pamoja na muziki wa kizazi kipya mkoani mwanza wameliomba baraza la taifa la sanaa (BASATA) kufungua ofisa zake jijini mwanza ili kuwaondolea adha ya kufuata huduma zinazotolewa na baraza hilo jijini dar es salaam.

Wasanii wa aina mbalimbali wakiwemo wa filamu, ngoma za asili pamoja na kizazi kipya wakiwa wamekutanishwa na baraza la taifa la sanaa (BASATA) kwa ajili ya kusikiliza changamoto zinazowakabili kubwa ikiwa ni suala la maslahi.
Maombi ya kutaka BASATA ifungue ofisi mkoani mwanza ili kuwaondolea wasanii adha ya kusafiri kwenda kufuata huduma hizo jijini Dar es salaam yakawasilishwa na Rebeca pius ambaye ni mwimbaji wa muziki wa Injili kutoka Mwanza. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Kusanyiko la wadau wa sanaa Mwanza.
Mtayarishaji mkongwe wa muziki na video za wasanii Aron Mikomangwa amefunguka kuhusu nini kinakwamisha muziki na sanaa ya Kanda ya Ziwa kwa ujumla amesema wamekuwa wakitoa wito kwa wasanii kwenda shule bila mafanikio.

“Shida tuliyonayo ya wasanii wengi wa Tanzania tunafanya kazi ya sanaa bila kwenda shule,” alisema. “Somea hiyo sanaa shule tunazo, Bagamoyo, Butimba, University of Dar es salaam pamoja na nyuo vingine.”

“Lakini hatutaki kufanya, hatutaki kusoma ili tujue miiko ya sanaa ni ipi. Kila siku tunawaambia waende shule ili wafanye kazi professional, ndio maana wanaingia mikataba hawajui wanaingia nini. Waende shule, sanaa sio kitu cha kukurupuka, sanaa sio eneo la kukimbilia, it’s A professional, ni taaluma kama taaluma nyingine kwaHiyo lazima uende shule,” BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Malipo kidogo kwa wasanii wasio na majina na hata pengine kudhulumiwa kabisa wanaposhirikishwa na wasanii wakubwa wa Bongo Movie hili ni kilio cha wasanii wa filamu Mwanza.
Serikali inapenda kuvuna toka kwa wasanii lakini haiko radhi kujitoa kuwasaidia wasanii. Mtayarishaji wa filamu Mwanza akitema chache kwa BASATA. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Kusanyiko la wadau wa sanaa Mwanza.
Kusanyiko la wadau wa sanaa Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.