ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 19, 2017

WATU WATATU WAFARIKI DUNIA PIA RPC MWANZA ADHIBITISHA KUTEKWA KWA WATOTO 3 NA MWANAMAMA RAIA WA CONGO.


Hii ni moja kati ya habari zilizotikisa:- Watu watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti.

Katika tukio la kwanza wawili kati yao wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa baada ya nyumba ya Afisa Ustawi wa jamii Buchosa wilayani Sengerema kuteketea kwa moto.

Pata taarifa hii na nyingine ya utekaji watoto:-
Mama mmoja aliyetambulika kwa jina la Asia Ismali alimaarufu kama Apendeki Katembo Rashid mwenye umri wa miaka 37 raia wa Congo anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuiba watoto watatu Nyamagana Mwanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi linamshikilia mama huyo kwa tuhuma za kuiba watoto watatu, wawili wakiwa na umri wa miaka mitatu na mmoja akiwa na umri wa mwaka mmoja na nusu.


 BOFYA PLAY KUMSIKILIZA KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mwanza, Ahmed Msangi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.