ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 6, 2017

MYANMAR YATEGA MABOMU ARDHINI KATIKA MPAKA NA BANGLADESH KUWAZUIA WAISLAMU KUONDOKA.

Myanmar yatega mabomu ardhini katika mpaka na Bangladesh kuwazuia Waislamu kuondokaInaarifiwa kuwa serikali ya Myanmar inatega mabomu ya ardhini katika mpaka wa nchi hiyo na Bangladesh ili kuwazuia Waislamu wa kabila la Rohingya kuondoka nchini humo.

Vyanzo viwili vya habari nchini Bangladesh vimeliambia shirika la habari la Reutrers kuwa, mbali na kutega mabomu ardhi, kadhalika vyombo vya usalama vya Mynmar vimeweka uzio wa nyaya katika mpaka huo ili kuwazuia maelfu ya Waislamu hao kuondoka.

Manzurul Hasan Khan, afisa wa Gadi ya Mpakani amesema watoto wawili wa Kirohingya wamejeruhiwa katika mripuko wa mabomu hayo huku mwanamke mmoja akipoteza mguu wake.

Waislamu wa Rohingya wakikimbilia Bangladesh.
Duru za habari zinasema kuwa, serikali ya Dhaka inatazamiwa kutoa malalamiko rasmi hii leo kuhusu mabomu hayo katika mpaka wake na Myanmar. 

Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia Waislamu wa jimbo la Rakhine, ambapo zaidi ya 400 miongoni mwao wamekwishauawa, huku wengine zaidi ya laki 1 na 25 elfu wakikimbilia Bagladesh.

Mauaji na jinai hizi zinafanyika mkabala wa kimya cha taasisi husika za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.