Kinara wa Muungano wa Upinzani wa NASA nchini Kenya, Raila Odinga katika moja ya mikutano yake na wandishi wa habari. |
Kesi inayopinga matokeo ya urais nchini Kenya
imeanza kusikilizwa rasmi na mahakama ya juu zaidi nchini humo hii leo,
huku uapnde wa malalamiko ambao ni muungano wa upinzani ukianza utetezi
wake kwa saa tano.
Katika
siku ya kwanza ya kusikilizwa kesi hiyo mahakama kuu ya Kenya
imeiruhusu kambi ya upinzani NASA kuweza kusoma data za sava za Computer
za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC ili kufahamu namna ambavyo wizi ulivyotumika kupindisha matokeo ya uchaguzi uliopita.
Majaji wa Mahkama ya Kilele nchini Kenya wakisikiliza kesi
Majaji wa Mahkama ya Kilele nchini Kenya wakisikiliza kesi
Hii ni katika hali ambayo Kinara wa Muungano wa Upinzani wa NASA nchini Kenya, Raila Odinga
alikuwa mahakamani tangu mahakama hiyo ilipoanza kusikiliza keshi hiyo
bila kuondoka mahakamani.
Kwa upande wao mawakili wa upande wa chama cha Jubelee cha Rais Kenyatta wameitaka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa upande wa upinzani hauna ushahidi wa kutosha.
Kwa upande wao mawakili wa upande wa chama cha Jubelee cha Rais Kenyatta wameitaka mahakama hiyo kutupilia mbali kesi hiyo kwa madai kuwa upande wa upinzani hauna ushahidi wa kutosha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.