Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejea
wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu,
na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini.
Taarifa ya wapinzani wa Zimbabwe imeeleza kuwa, Mugabe hana
uwezo na nguvu za kuiongoza tena nchi hiyo hasa kutokana na kuwa
hospitali mara kwa mara.Gazeti la binfasi la News Zimbabwe limenukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC akisema kuwa, Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya. Ameongeza kuwa, hawezi kuiongoza nchi akiwa kitandani hospitalini.
Karauone Chihwayi, msemaji wa upande wa tawi lilijitoa ndani ya MDC naye ametoa matamshi kama hayo. Amebainisha kama ninavyomnukuu: Nchi hii imekwama kwa sababu rais wa ZANU-PF anaongoza akiwa katika kitanda cha hospitali."
Rais Ribert Mugabe wa Zimbabwe. |
Wito wa wapinzani wa kumtaka Rais Mugabe ajiuzulu umekuja masaa
machache baada ya kuripotiwa kwamba, kiongozi huyo wa Zimbabwe yuko
nchini Singapore kwa ajili ya matibabu, hii ikiwa ni safari yake ya tatu
ya kitiba nchini humo mwaka huu.
Pamoja na kuwepo wasiwasi kuhusu hali yake ya afya, Mugabe amesafiri
mara 10 nje ya nchi mwaka huu na safari yake ya mwisho ya kikazi ilikuwa
wiki iliyopita wakati alipohudhuria kikao cha viongozi wa Afrika huko
Addis Ababa Ethiopia. Mugabe ambaye ameitawala Zimbabwe tokea
ijinyakulie uhuru kutoka Uingereza mwaka 1980 anasema atagombea tena
urais mwaka 2018.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.