Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 27 amekumbwa na mkasa huo baada ya Babu wa msichana huyo kuwakuta katika chumba cha darasa la shule anayofundisha mwalimu huyo wakiwa wanafanya mapenzi.
"Babu wa mwanafunzi alipoona mjukuu wake amechelewa kurudi nyumbani alianza kufanya msako, alikwenda kwenye shule ya sekondari lakini hakumuona ikabidi aendelee kumtafuta mjukuu wake, ilipofika kwenye muda wa saa sita na kitu alikwenda kwenye shule ya msingi ya Mabomba katika moja ya darasa wakakuta huyo mwanafunzi wa kike akifanya mapenzi na mwalimu wa shule hiyo ya msingi ya Mwabomba" alisema RPC Msangi
Msangi aliendelea kuelezea jinsi babu alivyoweza kuwakamata watu hao "Yule babu alikuwa ameongozana na watu wengine hivyo walipowaona waliwakamata wakaita na watu wengine, baadaye taarifa zilifika kituo cha polisi na polisi walikwenda na kuwakuta watuhumiwa hao kwenye lile darasa hivyo wakawachukua na kuwafikisha kituoni, hivyo mtuhumiwa yupo kituo cha polisi tunaendelea na mahojiano na taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea ili tuweze kukamilisha upelelezi tuweze kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo" alisisitiza Msangi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.