Baiskeli zimetumika kwenye maandamano Bujumbura |
Nchi za magharibi zinazofadhili Burundi zilighathabishwa na hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa muhula wa tatu, pamoja na kutumia nguvu kuzima maandamano.
Serikali pia imefuta ufadhili wake kwa Vyuo Vikuu na badala yake wanafunzi wote watagharamia ada za masomo punde wakiajiriwa baada ya kufuzu.Ada mpya za kuegesha katika jiji kuu ni dola mbili kwa baisikeli na dola 60 kwa malori makubwa.
Mamlaka zimetumia nguvu kuzima maandamano |
Mabasi ya uchukuzi wa umma yatalipa dola sita kwa mwezi. raia wengi wanahofia ada mpya huenda zikasababisha mfumuko wa bei ya bidhaa. Wakaazi wengi katika mji mkuu tayari wanalalamikia ongezeko la gharama ya maisha na wafanyikazi wengi hupokea dola 80 kwa mwezi.
Muungano wa Ulaya ulisimamisha msaada kwa serikali ya Burundi na kusema Mamlaka hazijasaidia kurejesha utulivu nchini.Msaada wa Muungano wa ulaya kwa Burundi ulikadiriwa kuwa dola milioni 470 kati ya mwaka 2014 hadi mwaka 2020.
Zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine laki mbili unusu kukimbilia katika nchi jirani kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyozuka baada ya Rais Nkurunziza kuamua kuwania mhula wa tatu.
Mwezi uliopita Burundi ilitangaza kujiondoa kutoka uwanachama wa mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.Tangazo hili lilitolewa miezi sita baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC kusema atachunguza ghasia nchini humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.