Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa katika dimba la Sokine kati ya Tanzania Prisons dhidi ya Simba umemalizika jioni ya leo kwa timu wenyeji kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Licha ya kufungwa Simba ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kunako dakika ya 43, mfungaji akiwa Jamal Mnyate, aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Shiza Kichuya
HALF TIME:
Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza cha mchezo huu. Timu zote zinaelekea vyumbani kupumzika.
Dakika ya 63: Prisons wanapata bao la pili, mfungaji ni yuleyule Hangaya, anafunga kwa kichwa na kwa staili ileile. Ilipigwa mpira wa pembeni mabeki wa Simba wakafanya uzembe, akaruka juu na kufunga.
Hadi dakika 90 zinamalizika mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania Prisons wanaibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba.
KIKOSI CHA SIMBA
1.Agban Vicent, 2 . Hamad Juma. 3.Mohamed Hussen, 4.Novaty Lufunga, 5 . method Mwanjali, 6 . Jonas Mkude, 7.Shiza Kichuya, 8.Mzamiru Yasssin, 9.Laudit Mavugo, 10.Mwinyi Kazimoto, 11.Jamal Mnyate.
Sub:
Peter Manyika, Emmanuel Simwanza, Said Hamis, Mohamed Ibrahim, Ndusha Mussa, Haji Ugando
KIKOSI CHA TANZANIA PRISONS
1. Andrew Ntala, 2. Salum Kimenya 3. Leonsi Mutalemwa, 4 . Jumanne Elfadhili 5. James Mwasote 6 . Kazungu Mashauri, 7. Lambarti Sabiyanka, 8. Mohamed Sammata 9. Victor Hangaya, 10. Salum Bosco 11.Benjamin Asukile
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.