ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 7, 2016

UTPC WAJIPANGA KUANZISHA CHAMA CHA WAFANYAKAZI WAANDISHI

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deo Nsokolo, akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC unaofanyika Jijini Mwanza kwa siku mbili, kuanzia leo Oktoba 06,2016.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali ikiwemo Mpango Mkakati wa UTPC kwa mwaka 2016/20 uliofadhiriwa na Shirika la Sida.
Na BMG
Viongozi wa UTPC wakiwa kwenye mkutano huo ambapo kutoka kulia ni Mkurugenzi wa UTPC, Abubakar Karsan, Rais wa UTPC, Deo Nsokolo, Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili UTPC
Wajumbe wa bodi, UTPC, wakiwa kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akiwa na wajumbe wengine kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kushoto) akiwa na wajumbe wengine kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mweka Hazina Mara Press Club akichangia jambo kwenye mkutano huo
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deo Nsokolo (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Mara Press Club, Mugini Jacob (kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa UTPC, Jane Mihanji (kushoto) kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Shinyanga, Kadama Malunde (kulia) akisalimiana na Rais wa UTPC, Deo Nsokolo (kushoto).

NA. ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza.

Umoja wa waandishi wa habari UTPC wajipanga kuanzisha chama cha wafanyakazi waandishi wa Habari tofauti na wamiliki vyombo habari pamoja kada zingine  kama madereva wao illi kutetea maslahi yao.

Akizungumza katika mutano wa dharula wa umoja huo jijini hapa Mkurugenzi wa UTPC Abbakar Karsan,  amesema chama hicho kitakuwa mahususi kusaidia na kuteteaq haki zao katika utendaji wa kazi.

Pia  Mkurugenzi wa huyo  amesema kufuatia mradi mpya ulioanza unaofadhiliwa na  SIDA wa nchi ya Uswis, uliwataka kuanzisha chama cha kuetetea waandishi walioajiriwa na ambao hawako kwenye ajira  na kwamba imekuwa ikitokea waandishi kutolipwa kwa kuwa wamiliki wanajua hakuna chombo kinachotete stahiki zao.

“Kwa miaka mingi UTPC imekuwa ikihangaika juu ya suala hili na utafiti unaonesha kuwa 80% ni waandishi wa kujitegemea na 20% ni walioajiriwa huku idadi kubwa wasioajiriwa ndio wanaotoa habari katika vyombo vingi kwa 90% tofauti na waajiriwa”alisema Karsan.

Aidha kwa upande wake Rais wa Muungano wa klabu za waandishi wa habari nchini Deogratius Nsokolo, amewataka waandishi nchini kuusoma na kuuelewa mswada wa huduma za habari ulio wasilishwa bungeni hivi karibuni kabla haujawachapa kufuatia kilichomo ndani ya mswaada huo.

Nsokolo amesema kuwa ni vyema wanahabari wakauelewa ili waweze kuchangia maoni yao juu ya mswada huo kabla haujawageuka endapo utapitishwa kuwa sheria.

“Huu mswada ni muhimu kwetu,na unatuathiri waandishi wa habari pamoja na kuwa wengi wetu tumejenga mazoea ya kusoma  vitu vya muhimu jujuu hatuelewi kwa undani zaidi na wengine hawasomi kabisa jambo ambalo ni hatari kwa tasinia yetu ya habari” Amesema  Nsokolo.

Mswada huo, uliwasilishwa Bungeni hivi karibuni na Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nauye ambapo waziri huyo alieleza kuwa  mswada huo ukipitishwa na Bunge kuwa sheria, utasaidia kuleta mageuzi makubwa katika taaluma ya habari na huduma za vyombo vya habari nchini bila kujua athari za baadae watakazozipata wathirika wa mswaada huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.