Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba
Hatua hiyo imekuja baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu, Sebastian Chinguka akipigwa kikatili na walimu.Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 28 baada ya mwanafunzi huyo kutofanya zoezi la somo la Kiingereza.
Zinaeleza kuwa walimu waliofanya kitendo hicho walikuwa kwenye mafunzo kwa vitendo.
Sasa baada ya sauti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba kusikila akilaani kile kilichotokea na kuapa kulifuatilia suala hilo Jembe Fm kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA Kinachoruka hewani kila siku saa 5 kamili hadi saa 7 mchana ilimtafuta Mwalimu Mkuu wa Shule kulikotokea sakata hilo.... BOFYA PLAY KUSIKIA KILICHOJIRI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.