Video ya wimbo mpya wa Crazy GK ‘Mzuri Pesa’ imetoboa mifuko yake kwa kiasi kikubwa, kwa mujibu wa yeye mwenyewe.
Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, rapper huyo aliyegeuka muimbaji, amedai kuwa alilazimika kuwasafirisha waongozaji wawili wa nje, mmoja wa Uganda na mwingine wa Afrika Kusini kwaajili ya kazi hiyo.
Amedai kuwa pamoja na gharama za kuifanya video hiyo, alilazimika kuwalipia gharama za hoteli kwa takriban wiki mbili.
Kingine amesema ni nguo zilizotumika kwakuwa alimpa kazi mbunifu wa mitindo kutengeneza nguo za wote wanaoonekana humo. Lengo la kufanya hivyo anasema ni kutengeneza brand yake kwa kutoa kitu bora. BOFYA PLAY KUSIKILIZA (SAUTI KUWAJIA HIVI PUNDE)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.