ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 2, 2016

WANANCHI ZAIDI YA 1000.WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA DARAJA MWANZA.

ZEPHANIA MANDIA MWANZA TAREHE. 02/08/2016. 

Wananchi wanaoishi katika kata ya Nyasaka A,B,NA C, wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa kivuko kiunganishi cha barabara yaani daraja katika mto Nyakurunduma ambao unatiririsha maji yake katika ziwa Victoria jijini Mwanza.

Wananchi hao wamesema tatizo hilo limekuwa kero kubwa ya miaka kwani mvua zikinyesha mto huo hufurika kiasi cha kusababisha wananchi kushindwa kuvuka maeneo hayo na wanafunzi kushindwa kufika shuleni kwa wakati au kukosa kabisa masomo wakishindwa kuvuka mto huo.

Wakizungumza na mwandishi wetu wamesema hivi karibuni wanafunzi watatu na dereva wawili wa pikipiki walisombwa na maji wakati wakivuka katika mto huo na kupoteza maisha.

Aidha wananchi hao wameongeza kuwa walipofikisha taarifa kwa mkurugenzi wa manispaa ya ilemela Bw. John Wanga, aliwahakikishia tatizo hilo analifanyia kazi baada ya mvua za masika kumalizika lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika badala yake wananchi hao wamelazimika kujenga daraja la miti ili wapate sehemu ya kuvukia kwani muda wowote mvua zinaweza kuanza tena.

Mananchi hao wamemlilia Mbunge wao Bi. Angelina Mabula kuwasaidia kutatua tatizo hilo ambalo limekuwa kero kabla mvua hazijarudi tena.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.