ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 3, 2016

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWA MTU WA KWANZA KUJIANDIKISHA KUSHIRIKI ROCK CITY MARATHON.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amekuwa mtu wa kwanza kujisajili kushiriki Rock City marathon inayotarajiwa kufanyika September 25 mwaka huu katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza. (BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI)

Akizungumza kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa mbio hizo mkoani Mwanza Bw. Mongella aliyekuwa ameambatana na Rais wa Chama cha Riadha cha Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mataka, pamoja na viongozi wengine wa mchezo huo ametoa wito kwa wadau wa mchezo huo mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kufanya jitihada za makusudi ili kuinua mchezo huo uliolipa Taifa heshima miaka ya nyuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John  Mongella (katikati) pamoja na Rais wa Chama cha Riadha cha Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mataka (wa kwanza kulia) wakishindana kujaza fomu za ushiriki wa Rock City Marathon ambapo mkuu wa mkoa wa Mwanza alimaliza mapema na kuwahi kuwasiisha kwa wadau wa mbio hizo hivyo kuwa mtu wa kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John  Mongella akizungumza na waandishi wa habari.
Rais wa Chama cha Riadha cha Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mataka akizungumza na vyombo vya habari kuhusu uzinduzi wa mbio za Rock City.
Rais wa Chama cha Riadha cha Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Anthony Mataka ametoa rai kwa Wadau mbalimbali wa majiji nchini kutumia mashindano hayo kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kwenye maeneo yao.
Wanahabari kwenye kusanyiko hilo.
Akizungumzia mbio hizo zinazoratibiwa na Kampuni ya Capital Plus International Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathews amesema kuwa mbio hizo zinafanyika mara ya nane mfululizo hapa mkoani Mwanza tangu zianze mwaka 2009 zikiwa na baraka zote kutoka Wizara ya Michezo, sanaa na Utamaduni, Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Chama cha riadha Tanzania pamoja na Chama cha Riadha Tanzania (MRAA)
Wadau wa uzinduzi.
Meza kuu.
Meza kuu na mazungumzo.




Picha ya pamoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.