Mshambuliaji wa timu ya JMK Park, Amour Gerald (kushoto) akimtoka mchezaji wa Vijana Sports, Omary Rashid katika mechi ya mashindano ya Airtel Raising Stars kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete Park. |
Mshambuliaji wa timu ya JMK Park, Amour Gerald (kushoto) akimtoka mchezaji wa Vijana Sports, Omary Rashid katika mechi ya mashindano ya Airtel Raising Stars kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete Park. |
Kiungo wa JMK Park, Marco Gerald akipiga mpira kichwa katikati ya wachezaji wa Vijana Sports katika mechi ya mashindano ya Airtel Raising Stars kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete Park. |
Kasulo yazidi kuzama Airtel Rising Stars
Timu ya Kasulo jana imedhihirisha kwa mara nyinginne kuwa ni ngazi ya kupandia kwa timu zinazoshiriki mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ilipokubali kipigo cha fedheha cha magoli 11-1 dhidi ya Bombom na kuufanya mchezo kuonekana mithili ya mechi ya mpira wa pete.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Jakaya Kikiwete Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam, ilianza kwa washindi kutalawa mchezo na kuwafanya wachezaji wa Kasulo kuonekana wasindikizaji.
Washambuliaji wawili wa Bombom Jamal Abdul na Saimoni Kazuya walikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kufunga magoli matatu kila mmoja hivyo kuweka kimiani jumla ya magoli sita peke yao. Magoli mengine yalifungwa na Masudi Hassan aliyefanikiwa kufumania nyavu mara mbili, huku Abubakari Said, Kishema Juma na Elia Nahdi wakifunga goli moja kila mmoja.
Goli na kufutia machozi la Kasulo lilipatikana kupitia kwa Anuari Amori ambalo hata hivyo hakuna mtu yoyote aliyelishangilia kwa kuwa lilifungwa kipindi cha pili ambacho tayari washabiki wa timu hiyo walikuwa wameshakata tamaa.
Hii ni mara ya pili kwa timu ya Kasulo kubebeshwa mzigo wa magoli kufuatia kipigo kingine cha magoli 9-1 walichokipata siku ya Jumapili walipocheza na Ilala Boys kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, rais wa kwanza wa Zanzibar.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mapema jana kwenye uwanja huo wa Jakaya Kikwete, JMK Park iliibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Vijana Rangers katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali na kuvuta hisia za watazamaji.
JKM Park walipata magoli yao kupitia kwa Marco Gerald mnamo dakika ya 15, Agiri Ngoda (dk 20) na Kapanga Jumanne (dk 46). Kwa upande wao, Vijana Rangers walifunga kupitia kwa Sefu Kwembe dakika ya 11 na Ramadhani Abubakari dakika ya 29.
Katika uwanja wa Tandika Mabatini, Carpert FC ilishinda 3-1 dhidi ya Kigamboni Soccer Academy ikiwa ni mchezo wa fungugua dimba katika mkoa wa kisoka wa Temeke.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.