ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 3, 2016

WANNE WAFA AJALINI WAKITOKA MSIBANI.


Dodoma. 
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Coaster walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye msiba kugongana na lori la Kampuni ya China katika kijiji cha Hamai, Wilaya ya Kondoa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 1.30 jioni wakati watu hao wakitokea kwenye msiba katika kijiji cha Paranga wilayani Chemba kwenda Moshi.

Alisema gari lililobeba waombolezaji hao lilikuwa likiendeshwa  na Daudi Hijabu wakati gari la Kampuni ya China lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina moja la Alfa.

Mambosasa aliwataja waliofariki ambao ni wakazi wa Mabogini, Moshi kuwa ni Abubakary Athuman (54), Hamida Juma (35) na Samira Amir (32).

“Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa lori, maana ilifikia mahali dereva wa Coaster alisimama lakini huyu dereva akamfuata na kumbamiza. Madereva wote walikimbia,” alisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.