Siku ya tukio mfungwa huyo Boniface Mwita (23) mkazi wa Kijiji cha Tamau wilaya ya Bunda mkoani Mara alikuwa akifanya usafi katika eneo la jeshi kikosi cha KJ27 kabla ya kupata upenyo na kutokomea kusikojulikana.
Baada ya kisa hicho polisi walifanya msako na kufanikiwa kumnasa akiwa nyumbani kwake Bunda na kisha kumfikisha mahakamani ambapo alikiri kosa la kutoroka. Baada ya kukiri kosa hilo hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Mara aliyesikiliza kesi hiyo Bw.
Adrian Kilimi akamuhukumu kwenda jela miaka mitatu tofauti na kile kifungo alichokuwa akikitumikia mwanzo. Mbali na hukumu hiyo askari mmoja ametiwa korokoroni kwa tuhuma za kumtorosha mfungwa huyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.