Makali ya agizo la kutokunywa pombe katika muda wa kazi yameendelea kuwaandama baadhi ya walimu katika shule za wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.
Safari agizo hilo limetoa makucha yake kwa walimu wa shule ya msingi Chifunfu katika Halmashauri ya Sengerema mkoani humo baada ya kukamatwa wakinywa pombe saa za kazi.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Chifunfu, Lucas Mashinji amesema walimu hao walikutwa baa Julai 29 saa 3.15 asubuhi, baada ya raia wema kutoa taarifa kwa diwani wa eneo hilo, Robert Madaha.
Mashinji amesema walimu hao wanashikiliwa ofisi ya kata wakisubuiri taratibu nyingine kufanyika.
Diwani Madaha alisema taarifa za walimu hao alizipata kutoka kwa wananchi kuwa walimu hao wapo baa hivyo alitoa maagizo wakamatwe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.