ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 2, 2016

AIRTEL YAINGIA UBIA NA NMB BANK KUONGEZA UFANISI KWA WAKALA WAKE.

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB ihudumie wakala wa Airtel Money.
Airtel Money yaingia ubia na NMB bank kuongeza ufanisi kwa wakala wake.
  • Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.

    Dar es Salaam jumapili julai 31 kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo popote nchini.

  • Akiongelea ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili wateja wetu wapate huduma za uhakika na  nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja wengi”

    Tunajisikia fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa huduma kwa lengo la  kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”

    “NMB itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso

    NMB na Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.