ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 9, 2016

SHAKA: KIKWETE AMETOA JASHO JINGI KUITUMIKIA TANZANIA


 Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa  tanga
Na Woinde Shizza,Tanga
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM )umevitaka vyama vya
upinzani wanaopika  maneno ya kipuuzi yenye  lengo la kuwagongajisha
viongozi wa CCM wakome na wamuache Mwenyekiti wa CCM  Dk Jakaya
Kikwete astaafu kwa heshima kwasababu ameitumikia nchi yake kwa kutoa
jasho jingi miaka kumi iliopita.

Aidha umoja huo umesisitiza kuwa kazi aliyoifanya Dk Kikwete katika
uongizi wake wa miaka kumi kisiasa na kiserikali utabaki kwenye vitabu
vya kumbukumbu ya historia iliotukuka hususan kila utakapokumbukwa
mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2015.

Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka ameyasema hayo wakati
alipozungumza na viongozi na  wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbi
wa TANU Hall mjini Tanga.

Alisema baada ya upinzani sasa  kujiona hawana hoja na hakubaliki
katika jamii maadui wa kisiasa wanotimiwa na nafisadi wamekuwa
wqkijaribu kupika uzushi na kutaka kuionyesha jamii kwamba viongizi wa
chama tawala hawana maelewano.

"Nakupeni  usia viongozi wa Ukawa ambao sasa mmekuwa wakiwa , mambo ya
ngoswe waachieni ngoswe wenyewe, viongozi wa ccm hawagombani,
hawajawahi kugombana na kamwe hawatagombana milele "alisema shaka
Aliwataka viongozi hao kutazama mustakabali wao kisiasa na kuachana na
ccm kwasababu chama hicho tawala haiwezekani kubomoka kwa maneno ya
jikoni , vijiweji au vichochoroni.

Shaka alisisitiza kuwa mwenyekiti wa ccm Dk Kikwete wakati akiwa Rais
ameitumikia nchi yake kwa kadri ya uwezo wake kama ambavyo
walivyotenda na kuitumikia nchi viongozi watangulizi wake akiwemo
baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee
Benjamin Mkapa na yeye ametenda kwa uwezo wake kama atakavyotenda Rais
Dk John Magufuli katika kipindi chake.

"Mtu mwenye akili timamu kila atakaposafiri akiizunguuka nchi yetu na
kupita juu ya barabara za lami, ujenzi wa madaraja, kutanuka kwa
mawasiliano, kukua uchumi wa Taifa na wa mtu mojmoja na wananchi iushi
katika nyumba za kisasa lazima utamkunbuka Kikwete taka usitake
"alieleza Kaimu huyo katibu mkuu .

Alisema kila zama ina kitabu na Nabii wake hivyo mema yaliofanywa na
kiongozi mmoja aliyemaliza muda wake yanahitaji kuheshimiwa kwasababu
Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni watoto wa baba na
mama mmoja.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.