Polisi wa usalama barabarani waliwahi kufika eneo la tukio na kulikuta gari hilo sehemu ya uso wake mbele likiwa limezama kwenye tope huku dereva wa gari hilo akijaribu kujinasua toka kwenye usafiri wake.
Gari hilo liliokuwa linaendeshwa na dereva ambaye jina lake linahifadhiwa, likiwa katika mwendo kasi dereva wake alishindwa kumudu kona kali ya barabara hiyo ambayo katika hali ya kawaida kwa sababu za kiusalama mwendeshaji yeyote anapaswa kupunguza mwendo kukabiliana na hatari yoyote inayoweza kujitokeza, lakini kinyume na hivyo suka wa gari hilo aliendesha kwa kasi hata kupata ajali.
Malumbano yalizuka baina ya askari na dereva ambayo yaliambatana na lugha chafu. Dakika chache baadaye askari wa jeshi la polisi wanaofanya doria eneo hilo walifika eneo hilo la ajali ambapo nao waliambulia kufurumushiwa matusi ya nguoni na vitisho toka kwa dereva huyo akidai kuwa watakiona cha mtema kuni mara baada ya so hilo kufika polisi ambapo kwa mgongo wa kujuana na baadhi ya watumishi wakuu atatoka tu ndani ya dakika sifuri.
Baadae dereva alisikika kutoa lawama kwamba anasikia maumivu, amedhalilishwa na kunyanyaswa kupitia kichapo cha mamwela hao naye akihidi kulipiza kisasi kwa aina yoyote ile namazingira yoyote.
Hadi kamera yako inatoka eneo la tukio hakuna ripoti yoyote ya majeruhi au kifo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.