Airtel yazindua Duka la kwanza katika Wilaya ya Kahama
Kampuni ya simu za Mononi ya Airtel Tanzania imeendelea na mikakati yake ya kusogeza huduma bora kwa wateja wake kwa kufungua duka lake la kwanza katika wilaya ya kahama Shinyanga
Duka hilo la kisasa ni moja ya ahadi ya Airtel kujali wateja wake Tanzania nzima na kuwapa huduma iliyobora na ya kiwango cha juu popote pale walipo.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa duka hilo, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel, Adriana Lyamba alisema, “ Airtel imefanikiwa kuwafikia wateja kwa kufungua milango mjini Kahama na kuwahakikishia tunaendelea kuwa wabunifu kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa zenye gharama nafuu kwa watumiaji wa simu za mkononi nchi
Duka hili ni la kwanza hapa mjini kahama, hivyo tunajisikia furaha sana kuleta huduma zetu karibu na wateja wetu na kuwapatia fursa ya kutumia huduma zetu kama vile Airtel Money kujiongezea kipato. Natoa wito kwa wakazi wa Kahama kupata nafasi ya kutembelea duka hili na kupata huduma pamoja na bidhaa mbalimbali ikiwemo modemu ya maajabu ya Airtel Wingle pamoja na simu orijino za smartphone kwa bei nafuu. Aliongeza Lyamba
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Bwana Vita Kawawa alisema “Kahama ni moja ya miji inayokuwa kwa kasi kubwa hivyo kufunguliwa kwa duka hilo kutaongeza ufanisi wa huduma za mitandano. Tunawashukuru sana Airtel kwa kuona ni vyema kutuletea huduma hii hapa mkoani na kutuhakikishia mawasiliano bora wakati wote na kuondoa changamoto zilizoko hapo awali. Kwa wakazi wa kahama huu ni wakati muafaka kutumia duka hili vyema ili kupata bidhaa zitakazotusaidia katika kuendesha shughuli zetu za uchumi na kijamii
Mpango huu wa Airtel kufungua maduka zaidi nchini, unalenga kuboresha maduka ya kampuni hiyo, ili yawe ya kisasa kama ilivyo katika mikoa ya mwanza, Arusha,Kilimanjaro na Mlimani City Dar es
Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.