ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 21, 2016

UKOSEFU WA DAWA KATIKA ZAHANATI MBALIMBALI NCHINI CHANGAMOTO KATIKA UHAMASISHAJI WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII.

Ukosefu wa dawa katika zahanati mbalimbali hapa nchini umekuwa changamoto katika uhamasishaji wa kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF na kusababisha wananchi kukata tamaa ya kujiunga na huduma hiyo kutokana na kukosa matibabu katika zahanati zilizo karibu yao.

Hivi umeshawahi kujiuliza kwanini wananchi wengi hukimbilia mijini kupata tiba?Jibu ni kwamba hata wakijiunga, sawa wanaweza kupata vipimo ikiwa ni pamoja na kumuona daktari lakini linapokuja suala la dawa inakuwa CHECHE. Hivyo baadhi yao wanarudi nyumba kwani hawaoni sababu ya kujiunga na mifuko hiyo ya bima ya afya.

Suala hilo limethibitika huko mkoani Mtwara katika mkutano wa wananchi na waelimishaji wa mfuko wa bima ya afya ambapo wananchi wamesema kitu kikubwa kinachowavunja moyo ni kutokana na ukosefu wa dawa wanapokwenda kutibiwa kwenye zahanati zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.