Airtel yainua kikundi cha vijana wajasiriamali kupitia Airtel Fursa jijini Dar es Salaam
· Airtel Fursa imewapatia pikipiki aina ya Guta, vifaa vya kutengenezea sabuni na vitendea kazi kwa vijana hapa nchini
Akili Mali ni kikundi cha vijana wajasiriamali 12 wanaojihusisha na biashara ya kutengeneza sabuni za maji za kufanyia usafi jijini Dar Es Salaam, ambao leo wamepokea vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA. Kundi hilI limepokea vifaa mbalimbali vikiwemo pikipiki aina ya Guta, vifaa vya kufungia sabuni, vifaa vya uzalishaji na vifaa vya usalama vya kufanyia kazi hiyo.
Meneja wa Airtel huduma kwa jamii bi, Hawa Bayumi aliwapongeza kundi la Akilimali kwa uvumilivu wao na kufanya kazi kwa bidii. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano alisema, "Airtel imeona sifa hizo na juhudi zao na ndio maana leo imewakabidhi vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi kwa haraka na endelevu ili kukuza biashara yao".
"Kikundi cha Akilimali kimeshapata mafunzo ya biashara ya ujasiriamali kupitia Airtel FURSA na wataendelea kupata ushauri na uongozi kutoka kwa washauri wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kuimarisha biashara yao " aliongeza Bayumi
Bayumi alielezea kuwa, "mwaka huu Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA umepanga kutumia zaidi ya bilioni moja kwa kuwawezesha vijana mbalimbali hapa nchini na kutoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia nafasi hii muhimu katika maisha yao.
"Kama kampuni ya simu inayojali jamii yake, tumeahidi kuwawezesha vijana hapa nchini kwa kuwawezesha kwa njia mbalimbali ili waweze kufikia ndoto zao.." alisema Bayumi.
Kwa upande mwingine kundi la Akilimali waliahidi kuweka ujuzi wao wote na kutumia kwa umakini vifaa vilivyotolewa kwao na Airtel kwa matumizi bora na yaliyo sahihi. Kiongozi wa kikundi hicho, Fatuma Rashidi, aliishukuru Airtel kwa msaada na kutoa wito kwa mashirika mengine hapa nchini kuiga mfano wa Airtel.
"Hatukuamini siku moja tutakuwa na uwezo wa kufikia malengo yetu katika biashara hii, tunaahidi kuweka juhudi zaidi na kutumia vifaa hivi na mafunzo tuliyopata kwa umakini zaidi kuhakikisha tunainua zaidi biashara yetu," alisema Fatuma.
Airtel FURSA, inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.