Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula, amewahakikishia Machinga Jijini Mwanza kuwa wataendelea kufanya biashara zao katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji hilo kama yaliyotengwa na uongozi wa halmashauri.
Mabula aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge wao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mbugani, kufuatia uvumi unaoezwa mitaani kwamba machinga pamoja na mamantilie wataondolewa katikati ya Jiji la Mwanza kufuatia ushindi wake.
“Mtu kaenda Makoroboi, Stand ya Tanganyika, Sahara, Soko la Igoma pamoja na maeneo mengine na kuwaambia Machinga na Mamantilie kuwa Mabula ameingia madarakani, cha moto mtakiona. Nataka msikilize kauli yangu leo kwamba sikuja kuitengua torati, nitaendelea kushirikiana na ninyi ili muwe bora, tena zaidi ya miaka mitano iliyopita”. Alisema Mabula.
Katika hatua nyingine Mabula amewashukuru wakazi wa Jimbo la Nyamagana kwa kumuamini na kumchagua kuwa mbunge wao, kwani wakati akiwa Mstahiki wa Jiji la Mwanza yeye pamoja na wanaccm wenzake walisemewa mambo mengi mabaya ambayo kimsingi hayakuwa na ukweli wowote.
“Akinamama walinyanyasika sana, walitemewa mate, walichaniwa nguo, walipondwa mawe, walitukanwa, walidharirishwa. Pia tulisemewa na kushuhudiwa uongo kila kona. Ninyi wenyewe mnakumbuka tuliambiwa tumevunja matorori, tumeiba maandazi , lakini nawashukuru maana wananchi wa Nyamagana walisema huyo huyo alieiba maandazi, kumwaga mchele na kuvunja matorori ndie atakuwa mtetezi wetu.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akimpongeza Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula baada ya kuhutubia na kutoa shukurani kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga ambaye pia ni mweyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mwanza, alipata nafasi kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliouonesha.
Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatu, aliwashukuru Watanzania wote kwa kukichagua chama hicho kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge pamoja na Rais ambapo Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 58.46
Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita ya Octoba 25 kote nchini, Mabula aliibuka mshindi katika Jimbo la Nyamagana kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumuondoa aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata Kura 79,280.
Baada ya mkutano huo wananchi walimsindikiza mbunge wao hadi kwenye ofisi kuu za wilaya ya Nyamagana zilizoko barabara ya Nyerere jijini hapa
Shangwe za wananchi wakiongozwa na akinamama wafanyabiashara wadogo na wajasiliamali....!!
Kitaa kwa kitaa.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula hapa alikuwa akiwaaga wananchi waliojitokeza kumsidikiza baada ya kumalizika kwa mkutano.
Mbele ya mjengo wa makao makuu ya CCM wilaya ya Nyamagana.
Hapa hapa pitiki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.