Mwenyekiti wa mtaa huo amesema wakazi wa mtaa wake wameathirika kwa kiasi kikubwa ambapo baadhi yao wameachwa bila makazi. BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Hili ni shamba la mpunga ambalo kwa sasa limegeuka kuwa jangwa mara baada ya mbegu zilizokuwa zimemea na kuchomoza kusombwa na maji kufuatia mafuriko. |
TMA imesema mvua hizo zinakuja kutokana na mifumo ya hali ya hewa kuzidi kuonyesha hali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a alisema jana katika taarifa kuwa maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka ya Dodoma, Singinda, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa, Njombe, Tabora, Kigoma Rukwa na Katavi zinatarajiwa kuanza kati ya wiki ya pili na ya nne ya mwezi huu.
Chang’a alisema mabadiliko hayo yamesababisha mwitikio wa mfumo wa hali ya hewa katika Bahari ya Hindi kuwa na mchango hasi, kinyume na ilivyotarajiwa katika mwenendo wa mvua za vuli nchini kwenye kipindi Oktoba na kusababisha vipindi virefu vya upungufu wa mvua katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.
Kutoka jijini Mwanza, mvua kubwa iliyonyesha kuanzia alfajiri ilisababisha kufungwa kwa Uwanja wa Ndege na mwanafunzi mmoja kusombwa na maji.
Maeneo ya Mabatini na Kirumba ambayo hukumbwa na mafuriko mara kwa mara yalijaa maji na kusababisha watu kulazimika kuyachota ndani na kumwaga nje.
Mkazi wa Mabatini, Ronaida Mtatina alisema vitu vyake vilivyokuwa kwenye kibanda cha biashara vilisombwa na maji na vingine kulowana.
Mbali na hasara hizo mtu mmoja ameonekana akisombwa na maji kamaambavyo mwenzetu Mustapha Ramadhani alivyofanya mahojiano na shuhuda wa tukio hilo. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo alisema mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyamanoro, Zainab Shaaban (18) alisombwa na maji eneo la Nyamanoro wakati akivuka kwenda shuleni, lakini haijathibitika kama alifariki au la.
Hali ya eneo la kutua ndege uwanja wa ndege Mwanza. |
Hali ya eneo la kutua ndege uwanja wa ndege Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.