Oktoba 30,2015.
KAHAMA
Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga linawashikilia zaidi ya watu 10 kwa makosa mbalimbali waliyoyafanya wakati wa zoezi la upigaji kura katika Uchaguzi uliomalizika Oktoba 25.
Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha mkuu wa upelelezi wilayani Kahama George Bagyemu amesema watu hao wamekamatwa katika matukio tofauti yenye viashiria vya kuvuruga uchaguzi na uvunjifu wa amani.
Bagyemu ameyataja matukio hayo ni pamoja na la kuchomwa nyumba ya Sophia Joseph katika kijiji cha Butibu jimbo la Ushetu aliyetekeleza tukio hilo ni Shindai Lung’wecha chanzo ikiwa ni ushabiki wa siasa ambapo mtuhumiwa alikuwa upande wa CHADEMA na mhanga akiwa CCM.
Tukio lingine ni kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao kwa mgombea udiwani katika kata ya Ngogwa kwa tiketi ya CCM Kamuli Mayunga tukio lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 26 hata hivyo jeshi linaendelea kumsaka aliyetishia.
Ameongeza kuwa Katika kijiji na kata ya Kashishi jimbo la Msalala mgombea udiwani wa kata hiyo Samson Juma vyombo vyake vya usafiri viliharibiwa ikiwemo pikipiki yenye namba za usajiri T.137AXF kuchomwa moto pia gari lake SUZUKI T.702 BDX kupigwa mawe.
Hata hivyo watu 10 walioshukiwa kuwa na njama za kuharibu zoezi la uchaguzi lakini katika maelezo yao wamedai walikuja Kahama toka Dar Es Salaama kama mawakala wa CHADEMA walioletwa na aliyekuwa mgombea ubunge James Lembeli.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuwabaini watu wengine zaidi waliotekeleza matukio hayo na wakakimbia na uchunguzi ukikamilika litawafikisha Mahakamani kwa kuvunja sheria.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.