Mgombea huyo akiwapungia wananchi wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni hizo.
|
VICTOR MASANGU, KIBAHA VIKUNDI
KATIKA kuunga juhudi za serikali kupambana na kupunguza janga la umasikini linalowakabili vijana na wakinama Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala hilo endapo akichaguliwa awamu ya pili ambapo atatenga shilingi milioni 700 katika jimbo lake kwa ajili ya kuvisaidia vikundi vya ujasiriamali.
Mgombea huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni katika jimbo la Kibaha mjini ambapo amesema lengo lake kubwa ni kuvisaidia mtaji vikundi vyote vya ujasiriamali lengo ikiwa ni kuhakikisha anasaidia vikundi hivyo kuanzia ngazi zote za vijiji hadi jimbo.
Koka alisema kwamba anatambua katika jimbno lake la kibaha mjini kuna vikundi vingi vya ujasiriamali hivyo atahakikisha kwamba anaviwezesha katika kuvipatia mtaji kwa ajili ya kuweza kukuza uchumi wananchi wa Kibaha pamoja na Taifa kwa ujumla.
“Kwa upande wangu mimi endapo wakinipa nafasi ya kuongoza tena katika jimbo la kibaha mjini nitahakikisha kuwa ninashirikiana nao kw ahali na mali ili kuweza kuleta mabadiliko chanya kuanzia ngazi zote za kaya hadi ngazi ya Taifa kwa hiyo hiyo ndio moja ya mikakati yangu.
Pia alisema kwamba katika kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi ataweka mipango mikakati ya kuongeza viwanda vingi amabvyo vitaweza kutoa fursa ya ajira kwa vijana sambamba na kuongeza wigo mkubwa ya kuleta maendeleo kupitia sekta mbali mbali.
Aidha Koka alisema kwamba kutokana na kuwepo kwa changamoto kubwa ya uhaba wa maji ameshaanza juhudi za makusudi za kuweza kushirikiana na serikali kutandaza mabomba ili waannchi wa kibaha mjini pamoja na amneo mengine ya jirani waweze kuondokana na kero hiyo ya maji.
Aidha mgombea huyo amebainisha katika suala la kukuza uchumi atahakikisha analivalia njuga suala la miundombinu ya barabara ili kuweza kurahisiha shughuli mbali mbali za biashara kwa wananchi wake wa jimbo la Kibaha mjini pamoja na kuweka mikakati kaabambe kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ya kuongeza idadi ya zahanati na vituo vya afaya ili wananchi waweze kupata huduma kwa urahisi.
Mpaka sasa Mbunge huyo wa jimbo la Kibaha mjini katika kipindi chake cha miaka mitano iliyopita ameshavisaidia vikundi mbali mbali vya ujasiriamali zaidi ya 175 ambavyo ameshatumia gharama ya kiasi cha shilingi milioni 230.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.