Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa imemuwezesha mjasiriamali Prisca George Chillumba ambaye ni mmiliki wa biashara ya saluni mkoani Mtwara. Prisca amenufaika na mradi huu kwa kupatiwa vitendeakazi mbalimbali vitakavyomuwezezesha kupanua wigo wa idadi ya huduma zitatakopatikana katika saluni yake.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi amesema, sambamba na kuongeza idadi ya huduma zitakazopatikana katika saluni ya Prisca, vifaa hivi vitamuwezesha kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa wakati mmoja, jambo ambalo litamuwezesha Prisca kuajiri vijana wenzie ili kuendeleza biashara na kukuza kipato chake.
Bi Bayumi amesema, mpango huo wa kuwawezesha wajasiriamali unawapatia vitendeakazi vijana wajasiriamali ili kuwaongezea kasi ya maendeleo ya kibiashara vijana hawa ambao tayari wameshachukua hatua na kuanza kujishughulisha na biashara ndogondogo. Lengo likiwa ni kurudisha sehemu ya mapato yake kwa jamii katika njia inayoleta tija.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo.
Awali akipokea msaada huo Bi Prisca ameshukuru kwa vifaa hivyo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa.
“Siamini kama naweza kufikia malengo yangu katika biashra hii, naahidi kuongeza juhudi na kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara yangu lakini pia nitatoa fursa kwa viajana wenzangu” Alisema Priscar.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili waweze kukuza mitaji yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.