Meneja wa benki ya NMB tawi la Hai Medadi Malisa kulia akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule hiyo Teodora Mlayi huku akishuhudiwa na mgeni rasmi Zuhura Chikira ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Hai |
Meneja wa Benki ya NMB wilaya ya hai Medadi malisa Kushoto akiwa amekaa wenye madawati yaliyotolewa msaada na benki hiyo kwa shule ya msingi kambi ya Raha, kulia kwake ni Afisa Elimu wa wilaya hiyo Deogracia Mapunda akifuatiwa na katibu tawala Zuhura Chikira na mwenyekiti wa shule hiyo.
Na Woinde Shizza,Hai
BENKI ya NMB kanda ya Kaskazini imetoa msaada wa madawati 50 wenye thamani ya sh. milioni 5 katika shule za msingi Kambi ya Raha,iliyomo wilayani humo,huku msaada huo ukitokana na faida inayopata benki hiyo.
Akiongea jana baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki hiyo tawi la
Hai mkoa Kilimanjaro, Medadi Malisa alisema benki hiyo imeamua kutoa msaada huo kulingana na uhitaji wa shule hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa shule hiyo.
Alisema Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi ya uhitaji wa msaada kwa jamii lakini kwa kuzingatia na umuhimu wa eneo husika ndio maana imefikia uwamuzi wa kutoa madwati katika shule hiyo baada ya kutambua kuwa kuna haja ya kusaidia wanafunzi hao.
‘’ Benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 50 kutokana na uhitaji wa shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki yenu imetenga zaidi ya
shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo
kusaidia sekta ya Afya, Elimu na michezo,’’alisema Malisa.
Aliongeza kuwa kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya
wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa
bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya
sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.
"Msaada huu wa madawati umetokana na faida kidogo ambazo benki inapata
hivyo tumeona katika faida hizo ni jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa
ajili ya kuweza kuendeleza watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho,"
alisema Malisa.
Kwa upande wa Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Zuhura Chikira, ambaye
alimwakilikisha mkuu wa wilaya ya Hai aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa
msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki hiyo kwa kutoa
Alisema wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
upungufu wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya
shule za msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo.
Aliwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB, kwa uisaidia serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini asa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.