ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 3, 2015

JEH UMESHAMPATA RAIS WAKO?

KESHO Jumatano ya tarehe 4/06/2015 majira ya saa 10:00 asubuhi, ni siku ya kipekee kwa vijana kupata mwakilishi wao katika kinyang'anyiro cha kutangaza nia ya kugombea Urais kupitia CCM ambapo katika ukumbi wa Benki Kuu BOT Capripoint jijini Mwanza shughuli nzima itafanyika pale.

Kwa maana hiyo, GSENGO BLOG inakuahidi kukupeperushia video za matukio ya shughuli hiyo hatua kwa hatua.

William Mganga Ngeleja,(47 yrs old), Mbunge wa Sengerema tangu mwaka 2005, Mjumbe wa NEC(CCM), Mwanasheria kwa taalum, Wakili wa kujitegemea, aliyewahi kuwa Naibu Waziri kwa mwaka mmoja (Jan 2007-Feb 2008), na baadaye akawa waziri kamili kuanzia mwaka 2008-May 2012. 

Vipaumbele vyake:amani na utengamano wa kitaifa, kupiga vita ufisadi,rushwa na mmomonyoko wa maadili;kuboresha sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda, miundombinu, elimu hususan mikopo kwa wanafunzi, na huduma za jamii e.g maji na afya; ajira, ardhi, makazi bora, sanaa na michezo, kuimarisha Muungano na kuheshimu utawala bora. 

Pia atajielekeza kuboresha sekta isiyo rasmi,kodi za wafanyakazi,umuhimu wa sekta binafsi,usimamizi wa rasilimali za nchi, pamoja na kuimarisha mahusiano na jumuiya ya kimataifa. 

Kauli Mbiu yake- "Maono Sahihi,Mikakati Tulivu,Matokeo Halisi" (MMM). 

Ngeleja ni muasisi wa bomba la gesi Mtwara-Dar, miradi ya umeme kupitia REA, mwanzilishi wa utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja (fuel bulk procurement), alisimamia utungwaji wa sera mpya ya madini(2009), sheria mpya ya madini(2010).

Ndiye aliyetoa leseni kwa mradi mkubwa wa Mchuchuma na Liganga. 

Ngeleja anakumbukwa kwa kuboresha utaratibu wa kutenga maeneo na taratibu za mikopo na ruzuku kwa wachimbaji wadogo. 

Ndiye aliyeanzisha wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania(TMAA),ndiye aliyefufua shirika la madini la Taifa Stamico mwaka 2008. 

Na ndiye aliyeanzisha miradi lukuki kwenye sekta ya nishati ambayo inaendelea kutekelezwa hadi sasa! Ngeleja anakusudia kulipa jiji la Dar hadhi ya kipekee ili kutatua tatizo la foleni.

USIKOSE....!!

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.