ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, May 27, 2015

TIMU YA MAGEREZA YAWACHAPA BAKOLA 3-0 MICHUANO YA KOKA CUP NGAZI YA KATA YA NDEGE

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
TIMU ya soka ya Magereza FC jana imeweza kuibuka kifua mbele na kutawazwa kuwa mabingwa baada ya kuitandika bakola timu ya Yc Fc kwa mabao 3-0 katika fainali za michuano ya Kombe la Koka Cup iliyolindima kwenye uwanaja wa Kwa mbonde mjini hapa.
 
Katika fainali hiyo ya michuano ambayo imeandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvesery Koka kwa lengo la kuweza kufufua vipaji kwa vijana wa mitaani na kukuza mchezo wa soka, ambapo fainali hizo zilikuwa  katika  hatua ya ngazi ya kata ya picha ya ndege.
 
Mchezo huo wa fainali uliweza kuvuta hisia za mashabiki na wadau mbali mbali wa mchezo wa kandanda kutokana maeneo mbali mbali ya Wilayani kibaha pamoja ana pembezoni ili kuweza kushuudia maafande hao wa magereza jinsi wanavyolisakata kabumbu la aina yake.
 
Katika kipindi cha kwanza dakaka za mwanzoni timu zote mbili zilionekana kuingia kwa kucheza mpira wa kasi kutokana na kufanyiana mashambulizi ya mara kwa mara lakini wachezaji wa magereza waliweza kutumia nafasi yao vizuri kunako katika dakika ya 20 kwa bao pekee lililowekwa langoni na mchezaji Luselo John.
 
Bao hilo liliweza kudumu hadi katika kipindi kwanza kinaamalizika na kufanya timu hizo kwenda mapumziko huku magereza ikiwa ina mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa Yc Fc ambao  walionekena  kuingia uwanjani wakiwa na uhakika wa ushindi kutokana na kujiamini lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo.
 
Kipindi cha pili alikuwa ni yule yule mshambuliaji tegemezi wa timu ya magereza Luselo John  kuweza kubadilisha matokea kwa kuwainua mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo baada ya kuonyesha umwamba wake kwa kupachika kimiani bap la pili katika dakika 54 ya mchezo.
 
Hata hivyo kuingia kibindoni kwa bao hilo la pili kuliweza kuwafanya wachezaji wa Yc Fc kuanza kutupiana lawama wao wenyewe na wakati bado wanaendelea kujiuliza watumia mbinu gani ili waweze kuthibiti safu ya ushambuliaji wa timu ya magereza hali ilizidi kuwaendea kombo kutokana na kushambuliwa langoni mwao  kama nyuki.
 
Mchezaji Macho Goodluck wa kikosi cha magereza aliweza kuamua kufunga kalamu ya magoli kwa kufuli baada ya kupachika bao la tatu lililipatikana katika dakaka ya 70 na kuwaacha wapinzani wao wakiwa midomo wazi na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa bao 3-0.
 
Kwa matokeo hayo timu ya magereza iliweza kutawazwa rasmi mabingwa wa fainali hizo za Koka Cup na kuzawadiwa kiasi cha shilingi laki tatu pamoja na ngao huku wapinzani wao timu ya YC fc ambao walikamata nafasi ya pili wakijishindia shilingi laki mbili pamoja na ngao  na mshindi wa tatu ni timu ya Sore masela ambao walijinyakulia shilingi laki moja  na ngao. .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.