NA VICTOR MASANGU, PWANI
SHIRIKA la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani limepata hasara ya kiasi cha shilingi zaidi ya milioni 12 kutokana na baadhi ya wateja wake nane kuhujumu miundombinu yake pamoja na kuiba umeme kwa njia ya kinyemela kinyume cha sheria na taratibu za nchi.
Hayo yamebanishwa na mkaguzi msimamizi wa shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Lugano Mwakinyala ambapo alisema kwamba wizi huo umebainika baada ya kufanya zoezi maalumu la ukaguzi wa miundombinu ya Tanesco katika Wilaya ya Bagamoyo.
Mwakinyala alisema kwamba kutokana na kukithiri kwa uharibifu wa miundombinu ya Tanesco pamoja na baadhi ya wateja wao kuwa na tabia ya kuiba umeme wakaamua kufanya ukaguzi ili kuweza kuwabaini wateja ambao wamekuwa wanatumia umeme mwingi kuliko gharama ambazo wanazilipia hivyo kulisababishia shirika hasara.
“Ndugu mwandishi nadhani wewe mwenye umeshuhudia jinsi ya miundombinu yetu ya tanesco ilivyoharibiwa hususan kwa upande wa mita zetu kwani wateja wameziharibu kwa kiasi kikubwa nah ii yote wanafanya hivyo ili waweze kuiba umeme na wanatumia gharama ndogo ukilinganisha na matumizi yenyewe,”
“Kwa mfano baadhi ya wateja wetu katika mita zao tumekuta waya ambao unatakiwa kwenda kwenye mita wao wameufanyia utundu ili usiweze kusoma katika mita na badala yake wameupitisha moja kwa moja katika soketi ili matumizi ya umeme yaw e chini kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria,”alibainisha Mwakinyala.
Aidha Mwakinyala akizungumzia kuhusisna na athari ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na wateja wake kuiba umeme pamoja na kuchezea mita zao na miundombinu ya Tanesco bila kuzingatia tartibu kunaweza kujitokeza kwa majanga mbali mbali yakiwemo kuungua kwa nyumba.
Pia alibainisha kwamba katika baadhi ya maeneo kumekuwepo kwa majanga ya moto ambayo yamekuwa yakijitokeza lakini sababu kubwa inayopelekea ni kutokana na wateja wao kuamua kujiunganishia umeme wenyewe kitu ambacho amedai ni hatari kwa sana kwa maisha yao.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kuachana kabisa na tabia ya kujishughulisha na uharibifu wa miundombinu ya Tanesco pamoja na wizi wa umeme kwani watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani ili iwe fundisho kwa wateja wengine.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.