ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 8, 2014

WATAALAM BINGWA KUTOKA FINLAND WAMPINGA WAFANYABIASHARA KURUHUSIWA KUZAGAA TENA KATIKA MITAA KATIKATI YA JIJI










PETER FABIAN, 
MWANZA.
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Murongo, amevuruga   utaratibu na    kuvunja sheria za Mipango Miji za Jiji la Mwanza na kusababisha wafanyabiashara wadogo maarufu “Machinga” kufanya biashara kiholela katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Hatua ya RC Murongo ya kuutaka uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutowaondoa wafanyabiashara “Machinga” waliozagaa kila mahali katikati ya Jiji hilo,    kumechangia Jiji la Mwanza, kushindwa kutekeleza jukumu la usafi na mazingira, kuwapanga katika maeneo yaliyotengwa na kupitika kilahisi.

Mkuu huyo aliyehamishiwa hivi karibuni akitokea Mkoa wa Arusha alitoa kauli tata hiyo alipofika katika ofisi za Mkuu Wilaya ya Nyamagana kujitambulisha na kuzungumza na viongozi, watendaji wa Halmashauri na watumishi, jambo ambalo limeonekana kulalamikiwa na wafanyabiashara wakubwa na baadhui ya taasisi za madhehebu ya kidini.

Hatua hiyo pia imeonekana pia kupingwa na wataalamu bingwa Kaj Heinio na Erkki Ottela kutoka Jiji la Tampere la Finland walikuja kutoa mafunzo ya mfumo wa ushirikishwaji wa jamii katika sekta binafsi kwa wajasiliamali wadogo, kati na wadau wa biashara ikiwemo taasisi mbalimbali zilizopo Jiji la Mwanza kwa madai kuwa Jiji
likiwa na wafanyabiashara holele halitakuwa safi na linalopanginka.

Heinio alisema kuwa uwepo wa wafanyabiashara wadogo si tatizo bali kufanya shughuli zao katika maeneo yasiyorasmi na kutengwa kwa shughuli za biashara ndogondogo katikati ya Jiji kunasababisha Jiji kupoteza sifa na uhalisia wa hadhi ya Jiji ambalo linazingatia taratibu na sheria za mipango miji kimataifa.

“Hali hii pia inaweza kuwaogopesha wawekezaji kuja kuwekeza katika Jiji ambalo halina utaratibu na mpangilio mzuri, pia kuhofia amani na usalama wa wafanyabiashara wakubwa na watalii wanaolitembelea kuhofia kupoteza mali zao endapo zitazuka vurugu wakati wa kuwaondoa kwenye maeneo kutakakofanywa na Halmashauri husika”alisema. 

Naye Ottela alifafanua kuwa kiongozi huyo wa serikali ni vyema akazingatia utekelezwaji wa sheria pamoja na kuonya wanasiasa kuacha kuingilia majukumu ya utekelezaji wa sheria kutokana na wanasiasa hao kutumia muda mwingi kuwapotosha wananchi kwa masilahi yao ya kisiasa.

Kwa upande wake Elirehema    Kaaya, kutoka ofisi ya Afisa Mahusiano wa Jiji la Mwanza alisema kuwa pamoja na kauli ya Mkuu wa Mkoa Murongo wapo pia baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitaka kuungwa mkono na kundi hilo la machinga, mamalishe na bodaboda kwa kupinga Halmashauli kuwaondoa na kuwapanga kwenye maeneo yaliyotengwa.

Utamsikia mwanasiasa akitumia jukwa la siasa katika mikutano ya hadhara kwa kuzungumza bila woga kuwa askari na mgambo wa Jiji acheni kuwasumbua wapiga kura wangu hasa hawa wamachinga na mamalishe jambo ambalo Halmashauri inapotekeleza kuwaondosha hutokea vurugu na uharibifu wa mali za wananchi”alisema.

Naye Donald Kasongi alitowa wito kwa wananchi kutolalamika kila wakati na badala yake lazima jamii ikubali kubadilika na kuzikubali sheria za Halmashauri na zile za nchi ili kutoleta mgongano wakati wa utekelezwaji wake, pia kuwa makini na kauli za wanasiasa hali inayoweza kuleta machafuko na kushindwa kutii sheria bila shuruti.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.