ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 9, 2014

CLOUDS 14 YATEMBELEA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MWANZA.

Msimamizi mkuu wa mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, Injinia Zuma (katikati) akiwa na Bonge wa Clouds fm (kulia) na Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Joseph Mlinzi (kushoto) kwenye eneo la mradi Ghana jijini Mwanza.
Msimamizi mkuu wa mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, Injinia Zuma akiwa kazini kwa shughuli zake na majukumu ya asubuhi kila kunapo kucha.


Mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex, pindi utakapo kamilika utakuwa na mwonekano huu.

Muonekano kwa ndani.
Huu ni ujenzi wa mradi wa ujenzi Soko la Kisasa la Mwanza (Mwanza Commercial Complex), ambao tayari umekwishaanza takribani miaka miwili sasa na umefikia katika hatua hii nzuri.

Mradi huu wa ujenzi wa kitenga uchumi hiki, unaendeshwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakati Jiji hilo halijagwanywa kuwa pande mbili, na Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF). Mradi huo unajengwa eneo la Ghana, katika Kata ya Nyamanoro iliyoko ndani ya mipaka ya Manispaa ya Ilemela.

Watanzania wazalendo wa nchi hii ndiyo watakao pewa kipaumbele kuwekeza biashara katika mradi huu wa mwanza Commercial Complex.

Na mradi huu, hadi utakapokamilika, unakadiriwa kugaharimu Sh bilioni 60.45.
Moja kwa moja na muonekano engo nyingine ya katika ujenzi.
Wadau wakiwa katika la juu la mjengo huo wa mradi.
Hakuna haja ya kubeba vifusi vya zege na kupoteza muda, hii ni mashine ya kuchanganya zege iliyo na bomba maalim linalo safirisha zege hiyo hadi eneo la ujenzi kwa vitengo husika. 
Mjengo kwa mbele.
"Huu ni mradi wa Ujenzi wa soko la Kisasa la Mwanza Commercial Complex uliopo katika eneo la Ghana wilayani Ilemela jijini hapa, ambao pindi ukikamilika, hakika utatengeneza muonekano mwingine wa mvuto kwa jiji la Mwanza pengine hata eneo hili kugeuka kivutio cha utalii" Says Bonge wa Power Breakfast akihitimisha ziara yake jijini Mwanza ambapo pia alitembelea miji mbalimbali kanda ya Ziwa kama sehemu ya kuazimisha miaka 14 ya Clouds Fm.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.