Wanahabari kwanye kusanyiko la maandalizi. |
Kampeni hii ilianzishwa ikiwa ni matokeo ya mauaji ya wanawake yaliyotokea 1960 Mirabele Nchini Dominica, wanawake hao waliuawa wakiwa katika harakati za kupinga utawala wa kidikteta wa Rais wa nchi hiyo Ndugu Raphael Trujilo na kuhitimisha tarehe 10 Desemba ambayo ni siku ya kimataifa ya tamko la haki za kibinadamu, ikiwa ni ishara ya kuhusisha ukatili dhidi ya wanawake na haki za binadamu, kwani ukatili huu ni uvunjaji wa haki za binadamu.
Kwa kuona hivyo, MKUKI KANDA YA ZIWA wameamua kutumia fursa hiyo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, kupinga vitendo hivyo na kuhamasisha jamii kuchukua hatua pindi inapoona au kuhisi uwezekano wa kutokea kwa vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili kwa taasisi za kiserikali, taasisi za kiraia, jeshi la polisi na wnafamilia wengine wa karibu.
Bi. Khadija Liganga ambaye ni Ofisa Sera na Utetezi akifafanua jambo. |
Aina mpya ya ukatili wa kijinsia maarufu kama 'Memory card' unahusisha wanawake kuuawa na kunyofolewa sehemu za siri na umekuwa ukiripotiwa kufanywa na kundi la watu lililojiita Makhirikhiri na kuzua hofu kwa wakazi wa wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Tukio lingine ambalo limebaki kuwa simanzi na kuwekwa katika historia ya matukio mabaya kutokea ni lile lililo msababishia ulemavu mwanamke mmoja huko mkoani Geita ambaye aliripotiwa kujeruhiwa kwa kukatwa mkono baada ya kuwepo kwa malumbano ya muda juu ya mazao yaliyopatikana shambani na kuuzwa na mume bila kumshirikisha mkewe huyo na baadaye mwanamke huyo kukatwa mkono na mumewe baada ya kuhoji.
Hii ndiyo Kamati ya Maandalizi ya Siku 16 za harakati za Kupinga ukatili wa kijinsia Kanda ya Ziwa. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.