ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 17, 2013

BIRTHDAY PART ILIYOVUNJA REKODI KUWA NA MAHUDHURIO MAKUBWA KULIKO ZOTE NCHINI YAFANYIKA MWANZA

Ni Birthday party ya mfanyabiashara mdogo Edward aliyetimiza umri wa miaka 27 akiwa ameketi na mama yake mzazi kwenye meza kuu. 
Sherehe hii ilihudhuriwa na watu 500 wakiwa waalikwa ambao walikuwa na kadi, wakapata chakula na vinywaji vya kujichagulia usiku huo, pamoja na wahudhuriaji wengine takribani 6,500 ambao walizamia shughuli hiyo bila mwaliko kutokana na eneo la tukio kuzungushiwa utepe kama uzio bila kuwa na kamati ya ulinzi wala mlinzi.
Lango la kuingilia ambapo kulikuwa na zuria jekundu (red carpet) ambapo ilikuwa ni fursa kupiga picha kwaajili ya kumbukumbu ya kuzaliwa Edward.
Shughuli ilifanyika katika moja ya viwanja vya shule ya msingi eneo la Igoma kukafungwa bonge la sound la mtikisiko, taa za uhakika na mapambo yenye ubunifu wa kila aina ambapo inatajwa wapambaji watatu maarufu jijini Mwanza walikula tenda kunakshi eneo husika. 
'Tumbuizo kali' Ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa msanii wa Bongo fleva Tunda Man ambaye alidrop jioni kwa pipa' hapa Rock City kwaajili ya shughuli moja tu... burudani 
Watu walivunja makabati kwani walipendeza haswaaa hadi wale walokuwa wazamiaji..
Ni kundi alikwa toka nyumbani Mwanza na mambo ya 'Azonto' 
Amini usiamini...Sherehe iliongozwa na kamati ya mtu mmoja tu! (pichani) ambaye ndiye alisimama kama Mwenyekiti wa kamati, mtunza fedha, mwenyekiti kamati ya ulinzi, mwenyekiti kamati ya Chakula, mwenyekiti wa kamati ya Vinywaji na sekta zote muhimu uzijuazo...balaaa.
Wageni waalikwa na vijiti midomoni ikimaanisha wamekula wakashiba na vinywaji tele mezani....
Safiiiiiiii..
Kuhusu mazazi ilikuwa ni full kulipuka uwezavyo. 
Burudani.
Jamaa alikamua Hip hop ragga ya hatari akichagizwa na madensa wake waliokuwa wakicheza kwa style ya tofauti kabisaaaa....
De nyu style...
'Tunakukubali' ni kama kauli ya mashabiki ...shereheni.
Starehe gharama...


Mzuka..!



Mwaga radhi...
Another Mc was Mr. Blue...Yooo...!
Mc mkali ngoma kali.....!
Hapo vije?...
Hatareee...!
minato ya Blue.
Mpala kuleeeee.....
Ze nyomi na area ya birthday ambapo ngoma ilikwenda mpaka saa tisa usiku mnene.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.